Usajili Ulaya Ulimwengu akamilisha mazungumzo na St.Etienne.
Wakati Mbwana Samata akiwekewa vikwazo kuondoka TP Mazembe, hali ni tofauti kwa Thomas Ulimwengu, ambaye yeye mambo yamemnyookea.
Mshambuliaji wa Klabu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu ameshakamilisha mazungumzo na Klabu ya Saint Etienne ya Ufaransa na kinachosubiriwa ni yeye kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo.
Ulimwengu amesema kabla ya dirisha dogo la usajili barani Ulaya kufungwa mwezi ujao tayari atakuwa ameshatua Ufaransa kuanza maisha mapya ya kusakata kandanda barani ulaya.
Ulimwengu ameileza StarTv kuwa mmiliki wa TP Mazembe, Mose Katumbi amebariki kuondoka kwake.
Ulimwengu ameweka bayana kuwa amechagua kwenda Saint Etienne kwa kuwa klabu hiyo inamsajili moja kwa moja bila kufanya majaribio.
Klabu ya Saint Etienne inayoshiriki ligi kuu nchini ufaransa kwa sasa inashika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa nyuma ya point 4 na timu ya Monaco inayoshika nafasi ya pili na point 34.
Hii ni kusema kwamba kama dili la Ulimwengu litakamilika na Saint Etienne ikamaliza nafasi ya tatu za juu basi Thomas Ulimwengu atakua Mtanzania wa kwanza kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya yaani UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Comments
Post a Comment