TWIGA ALIBINO APATIKANA TANZANIA,AWA GUMZO ,ASHANGAZA WENGI
Mwanasayansi
Dk Derek Lee amegundua twiga albino kwenye hifadhi ya mbuga ya
Tarangire iliyopo katika Mkoa wa Arusha nchini Tanzania.
Mtafiti
huyo Dk Derek Lee, alipiga picha mbalimbali zikiwa zinamwonyesha mnyama
huyo akiwa katika kundi kubwa la twiga, huku akiwa na rangi ya kipekee
ikilinganishwa na twiga wengine duniani.
Dk Lee, alimgundua twiga huyo wakati akifanya utafiti kwenye mbuga hiyo na nyingine za wanyama za barani Afrika,
Taarifa
iliyoripotiwa na shirika la habari nchini Uingereza kupitia gazeti la
Dailymail zimeeleza kuwa, twiga huyo adimu kupatikana duniani iwapo
atahifadhiwa atakuwa kivutio cha pekee katika mbuga hiyo.
Twiga
huyo anayejulikana kitaalamu kwa jina la ‘Omo’ likimaanishwa twiga
mweupe/mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino’, alionekana akizunguka katika
mbuga hiyo katikati ya twiga wengine. Dk Lee ambaye pia ni mtaalamu wa
viumbe na mwanzilishi na mwanasayansi kutoka Wild Nature Instute,
alimnasa twiga huyo katika kamera yake wakati akifanya uchunguzi huo
kuhusu wanyama.
Lee
(45) alisema: “Omo ni ‘leucistic’ hii inamaanisha seli zake nyingi
katika ngozi hazina uwezo wa kutengeneza rangi, hivyo anakuwa ni albino,
lakini hawi mweupe katika ngozi yake yote na wakati mwingine anakuwa na
macho mekundu au ya bluu kama ilivyo kwa albino.
“Ni
hali ya kimaumbile ‘Omo’ni aina pekee ya twiga ambaye anajulikana
duniani na ndiye pekee aliyeonekana Afrika kwa takribani miaka mitatu
sasa, pia tuligundua uwapo wa wanyama kadhaa wakiwamo nyati na mbuni
albino katika mbuga ya Tarangire,” alisema
“Omo
anaonekana kwa nadra sana na mara nyingi anapoonekana huwa pamoja
katika kundi kubwa la twiga wengine ambao huwa hawaonyeshi kushangazwa
na rangi aliyonayo.” “Kwa utafiti uliofanyika twiga huyo kwa sasa ana
umri wa miezi 15, aliishi mwaka wake wa kwanza kwa kunusurika kuuawa na
wanyama wakali kulingana na utofauti wake, kipindi ambacho ni cha hatari
kwa twiga wadogo hasa kutokana na kushambuliwa zaidi na simba, chui na
fisi ambao huwatafuna,” alisema.
Alisema
uwezekano wa twiga huyo kukua kwa sasa ni mkubwa, lakini bado wanyama
wakubwa wamekuwa wakimwinda na binadamu kwa ajili ya nyama za porini, na
huenda rangi aliyonayo inaweza kumfanya yeye kuwindwa zaidi.
“Sisi
na washirika wetu ambao wanafanya kazi katika mbuga mbalimbali na
wanaopambana na ujangili tupo kwenye mazungumzo ili kumsaidia Omo huyu
na wengine watakaopatikana kuhifadhiwa vizuri ili waishi kwa muda mrefu.
Tunaimani kwamba wataishi miaka mingi na baadaye atazaa na kupata
watoto watakaofanana na yeye na hivyo kuongeza vivutio vya twiga weupe
duniani,” alisema Dk Derek.
Imetafsiriwa na Herieth Makwetta, kwa msaada wa mitandao mbalimbali ya kimataifa-
Comments
Post a Comment