KUVISHWA PETE YA UCHUMBA, SIRI 3 KILIO CHA LULU ZAFICHUKA
Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuvishwa pete ya uchumba na Francis Shiza ‘Majizo B AADA ya wikiendi iliyopita staa ‘grade one’ wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuvishwa pete ya uchumba na bosi wa Radio EFM, Francis Shiza ‘Majizo’ na kuangua kilio cha aina yake, siri tatu (3) zimefichuka, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili. Kwa mujibu wa mtu aliyehudhuria, shughuli hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Majizo, Mbezi-Beach jijini Dar ilikuwa ya aina yake kwani watu walifurahi kwa kula na kunywa huku mastaa wa filamu wakionekana kutoalikwa au kutokuwepo. “Unajua ishu ya Lulu kuvishwa pete ya uchumba ilikuwa ni siri sana ndiyo maana hakukuwa hata na mastaa wenzake wa filamu zaidi ya mwigizaji Mahsein Awadhi ‘Dk Cheni’ ambaye alikuwa mshehereshaji lakini ilifana kwani mpaka Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alikuwepo,” alieleza mtu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini. SHEREHE ILIKUWA HIVI Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba sherehe ilianza vizuri