Tazama ‘FLYOVER’ Inavyofanya Kazi TAZARA
Septemba 15, 2018 daraja la juu ‘flyover’ lililopo katika makutano ya Tazara lilifunguliwa na magari yakaanza kupita na uzinduzi rasmi unategemea kufanywa na Rais Magufuli mwezi ujao.
Mradi huu ambao ni wa thamani ya Sh bilioni 95 unatekelezwa na kampuni ya Oriental Consultans Global na Eight Japan Engineering Consultants, zote za Japan.
Rais John Magufuli alizindua ujenzi wa ‘flyover’ hii Aprili, 2016 na kueleza kuwa lengo ni kupunguza kero ya foleni jijini Dar es Salaam pindi itakapomalizika na kuanza kutumika.
GLOBAL TV imefunga safari mpaka maeneo ya Tazara jijini Dar es Salaam kushuhudia ile barabara ya juu (FLYOVER) iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania ambao hivi sasa imesaidia kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa.
Baada ya kufika eneo la Tazara na kuona uzuri wa barabara hiyo na jinsi ambavyo magari yanapita, tukaamua kukielekeza kipaza sauti chetu na Wananchi wanaoishi kandokando ya barabara hiyo na kuwasikiliza wanalipi la kusema mara baada ya kukamilika kwa barabara hiyo.
Comments
Post a Comment