Mwili wa Dk Misanya Bingi waagwa Dar, kuzikwa Dodoma


MWILI wa aliyekuwa mtangazaji mahiri nchini na Mhadhiri wa Shule ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) iliyo chini ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi (47) umeagwa leo katika Kanisa Katoliki la Makongo Juu liliopo Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Mjini Dodoma kwa ajili ya mazishi siku ya kesho.

Dkt Misanya Bingi alifariki dunia siku Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wa uhai wake alifanya kazi kwenye kituo cha Radio One ambapo alitangaza vipindi mbalimbali kikiwemo kipindi cha Chemsha Bongo siku za Jumanne na Ijuma saa tatu usiku.

Hadi umauti unamkuta alikuwa akifundisha SJMC, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. na kabla ya hapo Misanya Bingi alikuwa mtangazaji kwenye kituo cha Radio One kazi aliyoanza kuifanya mwaka 1996.

Comments

Popular posts from this blog