Breaking News: Baba Mzazi wa Profesa Jay Afariki Dunia

       Profesa J.
MBUNGE wa Mikumi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Joseph Haule (Profesa Jay), amefiwa na baba yake mzazi leo akiwa katika Hospitali ya  St. Kizito,  Mikumi, ambapo alikuwa asafirishwe kwenda kupata matibabu zaidi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Prof. Jay amethibitisha kifo hicho katika mawasiliano aliyoyafanya kwa njia ya simu akiwa Dodoma.

Comments

Popular posts from this blog