Madiwani wapita bila kupingwa Uchaguzi mdogo wa Udiwani- Mbulu.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga akisoma taarifa ya maamuzi ya rufaa za Wagombea Udiwani katika kata za Tumati na Hayderer . Akiongea na vyombo vya habari hii leo ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mbulu, ndugu Hudson Stanley Kamoga amewatangaza Madiwani wawili wa kata ya Tumati ndugu Paulo Emanuel Axwesso (CCM) na ndugu Justine Sidamuy Masuja Hayderer(CCM),wamepita bila kupingwa baada ya Wapinzani wao kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa rufaa waliokata Tume ya Taifa ya Uchaguzi dhidi ya Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi. Msimamizi msaidi wa jimbo la Mbulu ndugu Michael Faraay(wa kwanza kushoto) akiwa na mratibu wa uchaguzi ndugu Stedvant Kileo wakimsikiliza kwa makini msimamizi wa uchaguzi (hayupo pichani)wakati wakusoma maamuzi ya rufaa Akitoa taarifa juu ya maamuzi ya rufaa hiyo iliyotolewa na tume ya taifa ya Uchaguzi,msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Wilaya ya Mbulu amesema amewaita wagom