Mshambuliaji wa Croatia atimuliwa Urusi, kisa kukataa kuivaa Nigeria



Mshambuliaji timu ya taifa ya Croatia Nikola Kalinic amerudishwa nyumbani baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu.

Kocha wake, Zlatko Dalic alimtaka mshambuliaji huyo kuingia katika dakika za mwisho katika mechi yao dhidi ya Nigeria, akagoma.

Kalinic aligoma akidai alikuwa na maumivu ya mgongo. Hivyo akakataa kuinuka na kuingia kama kocha huyo alivyotaka.

Pamoja na kwamba aliomba msamaha baada ya Croatia kushinda kwa mabao 2-0 katika mechi hiyo, Dalic alikataa katakata na kusisitiza, arejee nyumbani Croatia.

Comments

Popular posts from this blog