WIZARA YA AFYA YATANGAZA RASMI KUPOKEA HOSPITALI ZA RUFA ZA MIKOA
WIZARA ya afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018
imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya
usimamizi wa OR-TAMISEMI .
Hayo yamesemwa leo jijini Dar
es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya
Mwananyamala.
“Hospitali ambazo tumezipokea
zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao
Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni
182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya”
alisema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya
matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati alipofanya ziara ya
kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya
Mwananyamala.
Waziri Ummy amesema kuwa
Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya
Mount Meru (Arusha), Dodoma General (Dodoma), Kitete (Tabora),
Shinyanga, Geita, Singida, Mpanda (Katavi), Mawenzi (Kilimanjaro), Bombo
(Tanga), Morogoro, Ligula (Mtwara), Sokoine (Lindi), Maweni (Kigoma),
Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala, Amana, Temeke (Dar es Salaam),
Songwe, Kibena (Njombe), Iringa, Tumbi (Pwani), Sumbawanga (Rukwa),
Bariadi (Simiyu), Musoma (Mara), Songea (Ruvuma), Mbeya, Babati
(Manyara) na Bukoba (Kagera).
Waziri Ummy alisema kuwa
katika mwaka wa fedha 2018/19, Wizara imetenga shilingi Bilioni 30 kwa
ajili ya ukarabati wa miundombinu ya kipaumbele katika Hospitali za
Rufaa za Mikoa ambako tayari huduma zinatolewa ikiwemo Matibabu kwa
wagonjwa wa dharura ,Huduma za upasuaji wa dharura hususan wakati wa
ujauzito na uzazi pamoja na Huduma za tiba kwa wagonjwa mahututi
zikiwemo za watoto wachanga .
Mbali na hayo Waziri Ummy
amesikitishwa na upungufu wa wodi pamoja na vitanda kwa ajili ya
wanawake wanaofika kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya
Mwananyamala na kuahidi kulifanyia kazi mara moja iwezekanavo.
“Kama Mama,na nimeumia sana na
lazima tulifanyie ufumbuzi mara moja kwahiyo namuagiza katibu mkuu
alete mtaalamu wa majengo na tupandishe fedha za kujenga ghorofa mbili
mara moja kwakweli halii hii haikubaliki” alisema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza moja kati
ya wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala
wakati alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa makini
Bi Halima Said aliyefika kupata huduma za matibabu katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala pindi alipofanya ziara mapema leo katika
Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Bi.
Angelina Erasto juu ya umuhimu wa kukata Bima ya Afya ya TOTO AFYA KADI
itakayomsaidia kupunguza gharama za matibabu kwa mtoto wake,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akishangaa idadi kubwa
ya wakina mama iliyozidi kiasi katika wodi ya kupumzikia wakina mama
baada ya kujifungua, akiwa katika ziara yake ya kutembelea Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala kukagua ubora wa Huduma zitolewazo katika
Hospitali hiyo.
…………………….
Mnamo Novemba 25, 2017 Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) ya Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) aliagiza kuwa Hospitali
za Rufaa za Mikoa zihamishiwe kwenye usimamizi wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) kutoka Ofisi ya Rais
TAMISEMI.
Comments
Post a Comment