WIZARA YA AFYA YATANGAZA RASMI KUPOKEA HOSPITALI ZA RUFA ZA MIKOA
WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018 imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI . Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. “Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala. Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Hospit