Posts

MZEE MWINYI AONGOZA SWALA YA EID EL FITR DAR

Image
Mzee Ali Hassan Mwinyi akitoa nasaha zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu. Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia) akijumuika na waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika  swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum akitoa nasaha zake kwa waumini  wa dini ya Kiislamu. Taswira ya baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ilivyoonekana. Meneja wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akiwa ameungana na  waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja  vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (katikati) akisalimiana na mmoja wa waumini  baada ya kumalizika kwa swala ya Eid El Fitr. Sehemu ya waumini akinamama waliojitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja. Waumini wakiomba dua. RAIS Mstaafu wa Awamu ya P

Phars blogspot Inawatakia Eid Njema

Image
Wafanyakazi wote wa Kampuni ya Global Publishers & Ent. Ltd inayochapisha Magazeti ya Amani, Championi, Ijumaa, Risasi na Uwazi na Spoti Xtra tunawatakia heri ya   Sikukuu ya Eid El Fitr wadau na wasomaji wetu wote. Aidha tunawashukuruni sana sana wadau wetu wote kwa sapoti yenu kubwa mnayotupatia na kutufanya tuendelee kuwa namba moja kwenye tasnia ya habari za magazeti pendwa na michezo hapa nchini. Nasi tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi kwa asilimia zote.

MO SALAHA YUKO FITI KUWAVAA URUGUAY LEO

Image
HATIMAYE Kocha Mkuu wa Misri,Hector Cuper amesema mshambuliaji wa timu hiyo Mohamed Salah yupo kamili kwa takribani asilimia 100 kucheza mechi yao ya kwanza ya fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay leo Ijumaa, Juni 15, 2018. “Ninaweza kusema karibu asilimia 100 mchezaji Mo Salah yuko vizuri kucheza mchezo wa wetu dhidi ya Uruguay, yeye binafsi yupo tayari kucheza tunachojaribu sisi ni kumpa ujasiri tu”, amesema Cuper. Mohemed Salah aliumia bega kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Mei 26, kufuatia kukumbana na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos. Awali ilihofiwa kuwa huenda akakosa fainali hizo lakini sasa inaonekana yupo vizuri kuiwakilishi nchi yake. Misri ambayo ipo Kundi A na timu za Russia, Saudi Arabia na Uruguay leo itaanza rasmi kampeni ya kusaka ubingwa wa dunia ambapo haikupata nafasi ya kucheza fainali hizi tangu mwaka 1990 ambapo Salah alikuwa hajazaliwa. Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 9:00 Mchana kwa saa za Afrika Mashariki, kwen

Wanawake Urusi watakiwa kutofanya mapenzi na raia wa kigeni

Image
Mbunge mmoja nchini Urusi anasema kuwa wanawake hawafai kufanya mapenzi na wageni wakati wa kombe la dunia huku akionya kuhusu watoto wanaozaliwa kutoka rangi tofauti. Tamara Plentyova mkuu wa kamati ya familia, wanawake na masuala ya watoto bungeni, alisema kuwa hata iwapo uhusiano huo utasababisha kufanyika kwa harusi, wanawake au watoto wao watachukuliwa na nwanamume huyo ambaye atakuwa raia wa kigeni. Mbunge huyo ni wa chama cha Kikomunisti, ''Hata wakiolewa, watawachukua, halafu watashindwa namna ya kurudi," Bi Pletnyova alisema katika kituo cha Govorit Moskva. "Baadaye watakuja kwangu, wasichana wakilia kwamba watoto wao wamechukuliwa''. Alisema kuwa wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya 1980 mjini Moscow walisalia kuwa wanawake wasio na wanaume. ''Ni vyema iwapo ni mtu wa rangi inayofanana na yako lakini iwapo ni mtu wa rangi tofauti basi kunakuwa na shida''. ''

Ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh awamu ya pili waendelea kutekelezwa kwa zaidi ya aslimia 80- Mbulu

Image
muonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto kituo cha Afya Dongobesh likiwa katika hatua ya ukamilishaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu inategemea kukamilisha ujenzi wa majengo matano ya kituo cha Afya Dongobesh ifikapo Juni 30 2018, hatua hii imefikiwa ikiwa ni utekelezaji wa   kiwango cha aslimia 80 kilichobainishwa baada ya kufanyika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh,tathimini hiyo ilitolewa na   timu ya Wataalam toka Tamisemi, wakilishirikiana na wataalam toka   Mkoa wa Manyara .   Timu ya wataalam wakiwa katika moja ya majengo mapya ya kituo cha afya wakiendelea na ukaguzi. Timu hizo ziliweza kufanya ukuaguzi wa majengo hayo mapya yanayoendelea kukamilishwa kabla ya Mwezi Juni kukamilika ili kubaini kama   kiasi cha fedha Tsh.   Milioni 400   zilizotolewa   na Serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo unakamilika kwa wakati. Mgawao huo wa fedha uliotolewa ikiwa na mgawao awamu ya pili baada ya maeneo mbalimbali

Breaking News: Moto Mkubwa Waibuka Kariakoo

Image
Moto ukitekeleza ghorofa ya juu ya jengo hilo eneo la Kariakoo. MOTO mkubwa umeibuka Kariakoo katika mitaa ya Livingstone na Aggrey na unaendelea kuteketeza maduka. Tayari vikosi vya zimamoto vipo eneo la tukio kupambana na moto huo unaoendelea kuteketeza jengo la ghorofa ambalo lina maduka katika ghorofa ya chini. Moto huo ulianzia kwenye ghorofa ya kwanza katika jengo hilo lenye ghorofa mbili ambako kulikuwa na stoo ya vitu mbalimbali ambavyo vimeteketea kwa moto huo ambao moto huo ulielekea katika ghorofa ya juu. Chanzo cha moto huo hadi tunakwenda mitamboni kilikuwa hakijajulikana. Vikosi vya Zimamoto vikiendelea na kazi Wakazi wa Dar es Salaam wakishuhudia moto huo.

Je,wajua Rais Kim alisafiri na choo chake mpaka Singapore?

Image
Imebainika kuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisafiri na choo chake maalumu wakati wa mkutano wake na Rais Trump nchini Singapore. Sababu ya Kiongozi huyo kusafiri na choo chake imetajwa kuwa ni kuzuia kinyesi cha Kiongozi huyo kufanyiwa upembuzi na watu wa usalama wa mataifa mengine. Aidha imeelezwa kuwa Kiongozi huyo amekuwa na tabia ya kutembea na choo chake kila mahala anapokwenda kwani huwa hapendi kutumia vyoo vya umma. Kwa upande mwingine Kiongozi huyo alibeba gari lake aina ya Limousine ambalo halipitishi risasi pamoja na chakula chake mpaka nchini Singapore.

Ukeketaji Manyara yaongoza

Image
Hali ya Ukeketaji mkoa wa Manyara imefikia asilimia 70.8 kutoka asilimia 58 mwaka jana,hali ambayo ni mbaya zaidi licha ya jitihada za serikali na Mashirika binafsi kutoa elimu juu ya madhara ya kufanya ukeketaji. Hali ya Ukeketaji katika mkoa wa Manyara bado ni tatizo kutokana na watoto wachanga pia kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa siri pale wanapozaliwa. Anna Emmanuel Fisoo afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Manyara anaeleza kuwa tatizo la ukeketaji kwa wanawake na watoto bado lipo katika maeneo mengi ya mkoa katika baadhi ya makabila ya wafugaji. Amesema ukatili mwingine wanaofanyiwa watoto ni ulawiti na kubakwa na kwamba kesi nyingi zipo Mahakamani. Amesema ili kutokomeza ukatili huo ni lazima jamii,taasisi za serikali na mashirika binafsi kila mmoja atimize wajibu wake kwa wakati na kwa kufanya hivyo hali hiyo itakuwa imepungua kwa asiliamia 50 ifikapo mwaka 2022. Paskalia Changala Mratibu wa shirika linalojishughulisha na masuala ya kutokomeza ukeke

Lynn: Kuolewa na Diamond Wala Sina Papara

Image
Irene Charles ‘Lynn’ VIDEO Queen Irene Charles ‘Lynn’ ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema ametulia na hana papara kwani kama Mungu amepanga aolewe na msanii huyo, lazima itokee! Akizungumza na Risasi Jumatano, Lynn alisema, hawezi kuleta drama kwenye mitandao kuhusiana na suala lake na Diamond ila anachojua yeye kama Mungu amepanga aolewe naye, itakuwa hivyo na kama siyo basi ataolewa na mwingine aliyepangiwa. “Unajua siku zote ndoa hupangwa na Mungu hivyo kama Dai (Diamond) alipangwa kuwa wangu basi atakuwa wala sina papara, kama hajapangwa kuwa wangu atakuja mwingine,” alisema Lynn.

Tabia Ya Kuzoeana inavyoweza kuathiri Maisha yako ya kimahusiano

Image
Kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla. Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini. Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinn

Breaking News: Madrid Wamtangaza Lopetegui Kuwa Kocha Mpya

Image
Julen Lopetegui Klabu ya Real Madrid imemtangaza Kocha wa sasa wa Hispania, Julen Lopetegui kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo na atajiunga nayo baada ya mashindano ya Kombe la Dunia

Nape Nnauye: Bora mnilaumu kwa 'Bao la mkono' sio kwa hili la Jamii Forums

Image
Mbunge Mtama, Nape Nnauye amejikutaka akijibu hoja mbali mbali mtandaoni kufuatia mtandao wa Jamii Forums kusitisha kutoa huduma. Utakumbuka Jamii Forums wamefikia hatua hiyo kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018. Sasa Nape Nnaye alianza kueleza hisia zake kuhusu hilo kwa kuandika kwenye mtandao wa twitter; Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao….. kimya kimya!. Baada ya tweet hiyo idadi kubwa ya wachangia walionekana kuomnyooshea kutokana kipindi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipitisha sheria ya huduma za vyombo vya habari kwa mwaka 2016 Hata hivyo Nape aliwataka wachangia kutofautisha vitu hivyo kwani ni sheria mbili tofauti. “Nimeuliza hili swali toka mwanzo kina uhusiano gani wa hizi sheria mbili? Au tunakaririshwa au hatujui tunachotaka kusema,” alijibu Nape na mjadala kuendelea. Utakumbuka katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 2015 wakati Nape Nnaye akiwa Katibu Mwenezi

JPM Amwaga Tsh. Milioni 10 Cash Ujenzi wa Msikiti Dar

Image
RAIS John Magufuli ametoa pesa taslim kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mifuko 625 ya sementi itakayosaidi kwenye ujenzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA unaoendelea kujengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Rais ametoa mchango huo leo Juni 12, 2018 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti huo unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco. Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini Tanzania utabeba zaidi ya watu 8,000 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili au mei mwakani. “Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote,” amesema Rais Magufuli

UKWELI KUHUSU WANAFUNZI UDSM WALIOFARIKI DUNIA AJALINI

Image
TAARIFA zinazosambaa mitandaoni zikisema mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Maria Godian Soko amefariki dunia kwa ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Ubungo Riverside, Dar es Salaam, akiwa anakimbizwa hospitali kwa matatizo ya ujauzito, zimekanushwa na Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika chuo hicho, Hussein Amri Aman, aliyesema kwamba kwamba marehemu hakuwa na tatizo hilo. Amri amesema  marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu kwa muda mrefu,  hali iliyokuwa ikisababisha apoteze fahamu, na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa (ambulance). “ Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia, majira ya saa mbili kasoro usiku tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa Mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi” Ameongeza: “ Wakati taratibu za kumpeleka hospitali ya c

Historia Imeandikwa: Trump, Kim Jong Un Wakutana Live Singapore

Image
MKUTANO  wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani,  Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini,  Kim Jong Un,  umefanyika nchini Singapore. Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili  pekee yao na wakalimani wao. Mkutano huo ulianza kwa viongozi  hao wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao. Rais Trump amesema wawili hao wamepiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka za makubaliano. Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia. Hata hivyo, haijabainika ni nini kitakuwepo kwenye waraka ambao watautia saini. Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo. Mkutano uliokuw

Kafulila kuelezea sakata la Tegeta Escrow

Image
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema ataanza kuelezea kwa kina sakata lililotikisa nchi la kashfa ya Tegeta Escrow wiki ijayo kupitia gazeti la Uwazi. Akizungmza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Kafulila alisema amegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo wananchi wanataka kuyajua kuhusu sakata hilo, hivyo ameamua kuyaandika yote ili kiu ya Watanzania kujua kuhusu sakata hilo iishe. “Najua kwamba mimi ndiye niliyelibebea bango bungeni sakata lile na kwa kuwa Gazeti la Uwazi linasomwa na watu wengi, nimeamua kuyaeleza yote kupitia gazeti hili kuanzia toleo lijalo,” alisema Kafulila. Alifafanua kuwa wazo la kuandika sakata hilo amelipata baada ya kuulizwa sana na baadhi ya wananchi kwamba liliishaje na jinsi lilivyomfanya akorofishane na vigogo wengi na hata kujihatarishia maisha. “Kwa kuwa hilo ni jambo zito, ni vema wananchi wajiandae kusoma kwa urefu juu ya sakata hilo kwenye gazeti hili. Nadhani nimefanya uamuzi sahihi,” alisema Kafulila.

Ulinzi wa Rais wa Korea Kaskazini usipime

Image
Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore. Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote . Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka. Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji. Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri. Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi. Mwisho