U NAPO-MUONA mtu amefanikiwa kwenye uhusiano wake, amefunga ndoa na mwenza wake na kufanya sherehe, akili ya harakaharaka inaweza kukutuma uamini tu kwamba mambo ni rahisi tu. Kwamba walikutana tu mahali fulani, wakakubaliana na kuanza safari ya urafiki, uchumba na mwisho wa siku wakaingia kwenye ndoa. Bahati mbaya sana ni kwamba, unawakuta kwenye mafanikio. Unahisi pengine hawatumii nguvu nyingi kuendesha maisha yao na wanaelewana, hawagombani na kila uchwao wanafurahia maisha yao ya uhusiano. Ndugu zangu, licha ya kwamba kila mtu ana historia yake na wapo ambao huingia kwenye ndoa bila kupitia changamoto nyingi, lakini kikubwa ninachoweza kukuhakikishia mimi ni kwamba, changamoto ni lazima uzipitie ili uweze kufikia malengo yako. Tunafahamu kwamba kila mmoja anatamani aishi maisha mazuri yasiyokuwa na kelele, yasiyokuwa na misukosuko, lakini dunia ya wapendanao haipo hivyo. Mnakutana watu ambao hamjakua pamoja, mna tamaduni tofauti hivyo lazima mkumbane na chang