United Wamsajili Beki wa Porto

Beki Diogo Dalot

KLABU ya Man United imekamilisha usajili wa beki Diogo Dalot kutoka kwenye kikosi cha Porto cha Ureno.

Huu ni usajili mwingine wa kocha wa Man United, Jose Mourinho, ambaye anataka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 21, amejiunga na timu hiyo ya United kwa usajili wa pauni milioni 17.4 zaidi ya shilingi bilioni 37.


Akiwa na kikosi cha Porto, beki huyo alianza kucheza kwenye kikosi cha kwanza mwanzoni mwa mwaka huu na kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Dalot amesaini mkataba mrefu wa miaka mitano na timu hiyo ya England akiwa anaaminika kuwa atacheza kikosi cha kwanza chini ya kocha huyo Mreno.

United wanaamini kuwa beki huyo atamsaidia Antonio Valencia, ambaye ana umri wa miaka 33 na anaonekana kuwa anaweza akashindwa kuwika msimu ujao kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti mara kwa mara.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, anaweza pia kucheza kama beki wa kushoto na aliitumikia Porto kwenye mchezo ambao timu yake ilitoka suluhu na Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Alikuwa na msaada mkubwa kwenye timu ya taifa ya Ureno, ilipopata ubingwa wa Kombe la Euro la vijana chini ya miaka 17, ambapo alifunga mabao mawili, likiwemo moja siku ya fainali.

“Diogo ni kijana bora kwenye umri wake, ana kipaji cha kutosha kumuita beki bora kwa muda mfupi tu ni sawa kwa kuwa amekuwa mchezaji mahiri kwenye klabu yake.

“Ana kila kitu ambacho beki wa kushoto anatakiwa kuwa nacho, ana nguvu na ana uwezo wa juu wa kupambana uwanjani,” alisema Kocha wa United, Jose Mourinho.

Dalot ana kuwa mchezaji wa pili kwa United kusajiliwa baada ya hivi karibuni timu hiyo kumsajili Fred kutoka Shakhtar Donetsk ya Uturuki.

Comments

Popular posts from this blog