Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) , limefanya uteuzi wa wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bar a kwa mwaka 2018, kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria. Sanjari na uteuzi huo, JKT limewapangia Makambi ya JKT watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01-10 June 2018. Wahitimu hao, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, Nachingwea- Lindi na JKT Mtabila – Kigoma. Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya Ruvu JKT iliyopo mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia wa jamii hiyo. Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT w