Serikali Yalitaka Baraza la Maaskofu KKKT Kuufuta Waraka wa Pasaka

SERIKALI ya Tanzania imelitaka Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Tanzania kufuta waraka lililoutoa wakati wa mfungo wa kwaresma kwa madai kuwa Baraza hilo halina mamlaka kisheria ya kutoa waraka huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama, imesema kuwa imethibitisha kuwa uongozi wa Kanisa hilo umeshindwa kutimiza masharti ya usajili, kutoa taarifa za fedha na kutoa taarifa za mabadiliko mbalimbali kinyume na sheria.

Serikali imemtaka Askofu Mkuu wa KKKT kufika ofisi ya msajili ili apewe madeni na malimbikizo yake yanayopaswa kulipwa ndani ya siku 7 (kuanzia Mei 30, 2018).

Taarifa ya Serikali inaeleza kuwa Katiba inayotumiwa na Kanisa hilo ni ya mwaka 1960 ambayo ilipitishwa na msajili mwaka 1963. Hivyo Serikali inalitaka Kanisa hilo kuomba kibali cha kufanya marekebisho ya katiba hiyo.

Comments

Popular posts from this blog