Mwanafunzi aunda gari linalobadili jua kuwa Umeme


Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ameunda gari linalotumia kawi ya jua, gari ambalo limekuwa likiwavutia watu kutokana na kubadili jua kuwa umeme.

Samuel Karumbo, 30, ni mwanafunzi katika chuo cha mafunzo anuwai cha serikali mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya, amesema gari lake, ambalo lina mitambo mitatu ya sola iliyobandikwa, linaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 kwa siku.

Karumbo anasema mchana, sola huchukua nishati ya jua na kuibadilisha kuwa umeme ambao unahifadhiwa kwenye betri ambazo ndizo zinazotumiwa moja kwa moja kuliendesha gari hilo na pia wakati jua halijawaka sana.

Gari hilo lina uzani wa kilo 120 na kwenye mteremko hutumia mvuto wa nguvu za ardhi badala ya umeme. Nguvu hutumia tu kwenye kupanda milima au maeneo yenye miinuko.

Comments

Popular posts from this blog