BREAKING NEWS: KINANA ANG’ATUKA UKATIBU MKUU CCM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Kinana ameng’atuka katika nafasi yake hiyo ndani ya CCM huku Halmashauri Kuu ya chama hicho ikiridhia ombi hilo rasmi.

Hayo yamewekwa wazi na taarifa ilizotolewa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo Mei 29, 2018 na kusema kwa pamoja wamemtakia mafanikio mema katika shughuli zake.

“Napenda kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na CCM itaendeleaq kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadiri itakavyohitajika”, imesema taarifa hiyo.

Kwa upande mwingine, Kinana wakati anatoa neno lake la kuwaaga wajumbe wa NEC amewasisitizia wajumbe hao na wana CCM kiujumla kudumisha umoja wa wanachama na chama cha mapinduzi (CCM).

Comments

Popular posts from this blog