Nape atoa ujumbe mzito wa kumuaga Kinana

Mbunge wa Mtama, na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, Nape Nnauye amemaga na kumuahidi aliyekuwa Katibu wa chama chao, Ndg Abdulrahman Kinana aliyestaafu leo kuwa wataendelea kumuenzi na mbegu aliyopanda itaota.

Nape ametoa ahadi hiyo kwa Kinana ikiwa ni muda mfupi baada ya kiongozi huyo kutangaza kustaafu nafasi hiyo na kukubaliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Pamoja na hayo Nape ameweka wazi kumtambua kinana kama mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma.

"Pumzika rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi.  Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! Umepanda mbegu na itaota,"

Comments

Popular posts from this blog