WALIOISHIA VETA SASA WANAWEZA KUSOMA ELIMU YA JUU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) imethibitisha matumizi ya mtaala unganishi wa masomo ya ufundi nchini utakaowawezesha wahitimu wa vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi(Veta) kuendelea na elimu ya juu.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtaala huo,Mkurugenzi wa Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini,Dk Noel Mbonde amesema utasaidia kuwapa fursa vijana wengi waliotamani kuendelea na masomo ya ufundi ya juu kunufaika.
Amesema serikali inathamini maboresho hayo yanayotoa nafasi ya kuwanoa wataalamu wa kutosha inayoenda sambamba na sera ya serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa viwanda.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Standi
nchini,Dk Noel Mbonde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtaala Unganishi
katika Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)jijini Arusha ni Kaimu Mkuu wa Chuo
cha Ufundi(ATC),Dk Erick
Mgaya.

“Kulikua na tatizo la wanafunzi wetu wanaohitimu Veta kuendelea na kozi za juu za ufundi na sababu kubwa ilikua ni kukosekana kwa sifa za kuwawezesha
kujiunga na kozi za ufundi katika ngazi ya Stashahada na kuendelea mtaala unganishi umekua jibu,”alisema Dk Mbonde Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Erick Mgaya amesema mtaala huo ni matokeo ya mahitaji ya wahitimu wengi wa vyuo vya Veta nchini  kuwa
na shauku ya kuendelea na masomo ya juu ya ufundi.
Amesema kwa ushirikiano wa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sault nchini Canada walikamilisha mtaala huo unawapa sifa wanaotaka kuendelea na masomo kwa kuhudhuria kozi maalumu kwa muda mwa miezi mitatu.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi
Standi
nchini,Dk Noel Mbonde akizinduzi wa Mtaala
Unganishi unaowawezesha wahitimu wa Veta kuendelea na
elimu ya juu ya ufundi,kushoto ni Mshauri wa Ufundi kutoka Canada,Dk
Allan Copeland na kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi(ATC),Dk
Erick Mgaya

Mkurugenzi wa Ufundi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi
Standi
nchini,Dk Noel Mbonde akionesha Mtaala
Unganishi uliozinduliwa katika Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mshauri wa Ufundi kutoka Canada,Dk
Allan Copeland na kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk
Erick Mgaya
Naye Mratibu wa NACTE Kanda ya Kaskazini,Godfrey Komba amesema mtaala huo umekuja kwa wakati muafaka ambao serikali inahimiza matumizi ya teknolojia katika kusukuma ajenda ya uchumi wa viwanda nchini.
Aliwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo ya kupata elimu unganishi inayowapa nafasi ya kuendelea na elimu ya juu ya ufundi itakayofungua milango zaidi kwa kutoa nafasi ya kupata ajira kwenye makampuni makubwa na kujiajiri wenyewe.
Kwa upande wake Mshauri wa Elimu ya Ufundi kutoka nchini Canada,Dk Allan Copeland  amesema jumla ya wanafunzi 72 wameanza kozi unganishi katika Chuo cha Ufundi Arusha
kutoka mikoa mbalimbali ambao ni wahitimu wa vyuo vya Veta.

Comments

Popular posts from this blog