Posts

Mbwana Samatta Afanya Ziara Makka

Image
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, na mchezaji wa timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta (kulia) akiwa msikitini Makka. …Akiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya Genk,  Omar Colley. Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta,  anayekipiga katika timu ya Genk ya nchini Ubelgiji baada ya kumaliza msimu wa ligi kuu nchini humo,  ameelekea nchini Saudia Arabia kwa ajili ya kufanya ziara ya kidini huko Makka. Samatta anatarajiwa kurudi Tanzania mwishoni mwa wiki hii kujiandaa na mchezo wa hisani kati yake na mwanamuziki Alikiba katika mchezo wa soka utakaofanyika Juni 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa taifa kati ya Timu Alikiba dhidi ya Timu Samatta.

Kauli Ya Kitila Mkumbo Kuhusu Katibu Mpya wa CCM

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo. Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Bashiru Ally ni mtu sahihi kwa zama za sasa kuwa katibu mkuu wa chama hicho tawala. Jana Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, na kumpitisha msomi huyo ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano, kuwa katibu mkuu. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Profesa Mkumbo amesema , “katika kipindi ambacho silaha ya siasa ni nguvu ya hoja, weledi, na uimara CCM imepata katibu mkuu sahihi kwa zama sahihi nakutakia mafanikio makubwa komredi Dk Bashiru Ally.” Uteuzi huo umekuja baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuandika barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.

Kimenuka! Fumanizi la Mwezi Mtukufu Laibua Ndoa Mpya!

Image
Mke wa Sele Gogo, Shani ldd (mwenye dela lenye rangi nyekundu na nyeupe) akiwa na kundi lake nje ya chumba cha Mwajabu, KUNA mambo ya ajabu ya kila aina ambayo hutokea kwa nyakati tofauti, lakini hili lililojiri katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ni kali zaidi. Mke wa mfanyabiashara maarufu wa unga wa sembe mjini hapa, Seleman Husein almaarufu Sele Gogo aliyefahamika kwa jina la Shani Idd, anadaiwa kuzua timbwili zito katika tukio la fumanizi. Timbwili hilo la fumanizi linatajwa kutibua ndoa ya wawili hao kisha kuibua ndoa mpya kati ya Sele Gogo na mwanamke aliyedaiwa kufumwa naye, Mwajabu Juma ambaye baada ya kizaazaa hicho aliamua kufunga naye pingu za maisha. Kwa mujibu wa mashuhuda, fumanizi hilo lililojaza umati lilijiri kwenye chumba cha Mwajabu kilichopo Mtaa wa Makaburi B Kata ya Mji Mpya mjini hapa wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.     Sele Gogo na Mwajabu wakiwa kwenye pozi baada ya kufunga ndoa, Mashuhu

Nape atoa ujumbe mzito wa kumuaga Kinana

Image
Mbunge wa Mtama, na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, Nape Nnauye amemaga na kumuahidi aliyekuwa Katibu wa chama chao, Ndg Abdulrahman Kinana aliyestaafu leo kuwa wataendelea kumuenzi na mbegu aliyopanda itaota. Nape ametoa ahadi hiyo kwa Kinana ikiwa ni muda mfupi baada ya kiongozi huyo kutangaza kustaafu nafasi hiyo na kukubaliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. Pamoja na hayo Nape ameweka wazi kumtambua kinana kama mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma. "Pumzika rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi.  Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! Umepanda mbegu na itaota,"

MKE AMUUA MUMEWE KISA WIVU WA MAPENZI KAGERA

Image
Victoria Salvatory (58), mkazi wa kata ya Katoma, Kagera anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mumewe, Salvatory Iteganira (62) kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi amesema mauaji hayo yalitokea jana saa 6:00 mchana. Akizungumza leo Mei 28, Kamanda Ollomi amesema mtuhumiwa anadaiwa kumpiga mumewe kwa kitu kizito kichwani na kumsababishia jeraha lililovuja damu nyingi na hatimaye kifo. “Wanandoa hao wanadaiwa kuwa na ugomvi ambao chanzo chake tunaendelea kuchunguza; baada ya ugomvi huo mtuhumiwa alimpiga mume wake kichwani kwa kitu kizito kilichosababisha jeraha lililovuja damu nyingi na kusababisha kifo chake,” amesema Ollomi. Kamanda huyo amewaasa wanandoa na wapenzi kutumia njia ya majadiliano, usuluhishi na sheria kutatua tofauti miongoni mwao badala ya kujichukulia sheria mikononi. Matukio ya hivi karibuni ya mauaji ya wanandoa ni pamoja na la Muuguzi mfawidhi msaidizi wa hos

Maafisa wakuu wakamatwa kwa tuhuma za ufisadi.Kenya

Image
Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa nchini Kenya (NYS) Richard Ndubai, pamoja na maafisa wengine wakuu, wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za ufisadi. Hii inafuatia agizo la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma aliyeagiza kushtakiwa kwa washukiwa wote waliotajwa katika kashfa ya Shilingi bilioni 9. Maagizo ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma Noordin Haji yametolewa baada ya kupokea taarifa kuhusu kampuni 10 na pia zaidi ya watu 40 binafsi waliotajwa katika sakata hiyo NYS scandal kutoka kwa Mkurugenzi wa uchunguzi wa Uhalifu George Kinoti. "Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka ya Umma amechunguza nyaraka zinazohusiana na sakata inayoendelea katika NYS na ameagiza mashtaka yafunguliwe mara moja dhidi ya wite waliotajwa kushukiwa ," iliandika ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu asubuhi. Washukiwa wengine kadhaa pia wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani katika kipindi cha saa 24, kulingana na afisa mmoja katik

Kesiha Ateuliwa Mjumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM

Image
 MSANII wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya maarufu kwa jina la ‘Keisha’ ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (NEC) leo, Jumatatu, Mei 28, 2018.  Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kufuatia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho uliofanyika leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Keisha ambaye aliwahi kutamba kwa ngoma yake ya uvuymilivu na nyingine, aliwapi pia kuwania Ubunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Dodoma na kushinda katika kura za maoni. Kabla ya uteuzi huo wa leo, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.

BREAKING NEWS: KINANA ANG’ATUKA UKATIBU MKUU CCM

Image
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Kinana ameng’atuka katika nafasi yake hiyo ndani ya CCM huku Halmashauri Kuu ya chama hicho ikiridhia ombi hilo rasmi. Hayo yamewekwa wazi na taarifa ilizotolewa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo Mei 29, 2018 na kusema kwa pamoja wamemtakia mafanikio mema katika shughuli zake. “Napenda kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na CCM itaendeleaq kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadiri itakavyohitajika” , imesema taarifa hiyo. Kwa upande mwingine, Kinana wakati anatoa neno lake la kuwaaga wajumbe wa NEC amewasisitizia wajumbe hao na wana CCM kiujumla kudumisha umoja wa wanachama na chama cha mapinduzi (CCM).

Mbowe Afunguka Kauli ya Mwisho ya Bilago Kabla ya Kifo

Image
MWENYEKITI wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema maneno ya mwisho aliyoambiwa na aliyekuwa Mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, marehemu Kasuku Bilago kuwa alimwambia anahitaji msaada wa haraka wa matibabu. Akizungumza katika ibada fupi ya kuuaga mwili wa marehemu Bilago, Mbowe amesema wakati alipokuwa nje ya nchi, nchini Afrika Kusini Bilago alimtumia ujumbe kwamba hali yake kiafya si nzuri hivyo anahitaji msaada. “Nilipokuwa safarini nchini Afrika Kusini, mwalimu Bilago aliniambia ninaumwa hivyo naomba ushauri, nikawasiliana na bunge kuhusu taarifa yake ndipo walipomuamishia muhimbilli.Mwalimu aliliona hilo kwamba alikuwa anahitaji msaada wa haraka wa matibabu na kunitumia ujumbe nikiwa Afrika Kusini,” amesema Mbowe. Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa “Ndipo nilifunga safari Ijumaa, Jumamosi nilienda Muhimbili, nilimkuta hali yake imebadilika ghafla akakata kauli, nikaonana na madaktari ili wafanye juhudi za makusudi lakini walijaribu kwa muda wa nusu saa

Mkutano Mkuu wa CCM Mambo Moto

Image
MASIKIO ya wengi yameelekezwa kwenye mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika leo (Jumatatu) na kesho jijini Dar es Salaam, ambapo vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC ) vikitarajiwa kuwasha moto wa uamuzi mgumu unaotajwa kuwa ni nadra kutokea ndani ya chama hicho tawala. Tangu mkutano huo utangazwe ukifuatiwa na kutolewa kwa ripoti ya ya uchunguzi wa mali za CCM nchi nzima kumekuwepo na habari nyingi zinazohusisha uwezekano wa vikao hivyo kutoka na maazimio mazito, hata hivyo, chanzo kutoka ndani ya chama hicho kimeliambia Ijumaa Wikienda kuwa, agenda zake zitaleta mwangwi miongoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla. “Ni vikao vizito vitakavyoamua mambo mazito yenye faida kwa chama chetu, siwezi kusema ni yepi lakini tega masikio utasikia, CCM ni chama kikongwe na makini lazima mikutano yake hasa ya kitaifa iamue mambo makini .“Huwezi kuwa na chama kama hiki, kinachoshika dola halafu kiwe na mikutano ya kitotokitoto, wanaosema kitakuwa moto ni

Kijana aliyemuokoa mtoto ghorofani akutana na Rais, apewa uraia na kazi Serikalini

Image
Kijana raia wa nchini Mali, Mamoudou Gassam (22) ambaye Jumamosi iliyopita amefanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo ambaye alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nzito. Mamoudou amekutana na Rais Macron mapema Jumatatu hii kwenye Ikulu ya Elysee Palace kwa ajili ya kufanya mazungumzo pamoja na kupongezwa kwa msaada alioutoa. Rais Macron amempatia cheti cha Uraia wa Ufaransa kijana huyo ambaye alihamia nchini hapo kwa njia zisizokuwa za kihalali takribani miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kutafuta maisha, Lakini pia Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika jeshi la zima moto la Ufaransa. Kupitia mtandao wa Twitter Rais Macron ameweka picha akiwa Ikulu na kijana Mamoudou na kuandika, “With Mr. GASSAMA who saved Saturday the life of a child climbing 4 floors with bare hands. I announced to him that in recognition of this heroic act he would be regularized as soon as possi

TAJIRI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA, BASTOLA – DAR

Image
MAMLAKA ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewatia mbaroni watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, Ayoub Kiboko na mkewe, Pilli Kiboko, Mei 23, saa 8 usiku wakiwa nyumbani kwao eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam baada ya kuwasaka kwa muda mrefu. Kiboko ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara waliotajwa katika barua za Watanzania waliofungwa Hong Kong, ni maarufu ndani na nje ya nchi na anadaiwa kumiliki hoteli kubwa zaidi ya 10 pamoja nyumba za kifahari katika maeneo mbalimbali hapa jijini. Barua hizo zililetwa nchini Desemba 2014 na Kasisi John Wotherspoon anayesaidia wafungwa katika magereza ya Hong Kong na China na baada ya Watanzania hao kuandika barua hizo wakiwaasa wengine wasifanye biashara hiyo huku wakiwataja wafanyabiashara waliowabebesha dawa hizo za kulevya akiwamo Kiboko. Kamishna wa Operesheni DCEA, Frederick Milanzi alisema katika msako uliofanywa nyumbani kwake usiku wa manane, walimkamata Kiboko akiwa na dawa za kulevya

RATIBA YA SPORTPESA SUPER CUP HII HAPA KUNA ASILIMIA 90 SIMBA NA YANGA KUKUTANA NUSU FAINALI

Image
Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajia kuanza Juni 3 ,2018 kwa timu nane kushirikia ambazo zinadhaminiwa na Kampuni hiyo kubashiri Matokeo Bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda kucheza na Everton nchini Uingereza. Watani wa Jadi Simba na Yanga kuna uwezekano Mkubwa wakakutana Nusu Fainali ya Michuano hiyo huku Derby ya Mashemeji huenda ikatokea tena kama walivyokutana kwenye Fainali ya Msimu uliopita walipocheza uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Ratiba Kamili ni: Robo Fainali 03/06/2018 13:00 Kakamega Home Boys vs Yanga sc 15:15 Gor Mahia vs JKU 04/06/2018 15:00 Kariobangi Sharks vs Simba Sc 05/06/2018 15:00 AFC Leopards vs Singida United Nusu Fainali 07/06/2018 13:00 Winner (Gor Mahia vs JKU) vs (AFC Leorpard s vs Singida Utd) 15:15 Winner (Kakamega Home Boys vs Yanga Sc) vs ( Kariobangi Sharks vs Simba Sc) Mshindi wa tatu 10/06/2018 12:00 Loser Nusu Fainali Fainali 10/06/2018

Waziri Jafo atoa agizo hili

Image
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za  Mitaa (TAMISEMI),  Selemani Jafo, ameagiza  kufikia  mwezi Desemba mwaka huu taasisi zote za serikali katika halmashauri ya  jiji la Dodoma zinatakiwa kupata  hati miliki ya maeneo yao. Aidha,  ametoa muda wa mwezi mmoja kukamilishwa kwa ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo jijini  hapa ambacho kimeonekana kuwa ujenzi wake upo nyuma ikilinganishwa na vituo vingine 208 vinavyokarabatiwa nchini. Jafo alitoa maagizo hayo juzi mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo cha afya Hombolo iliyotolewa na Mganga wa kituo hicho kilichopatiwa fedha kiasi cha Sh. milioni 500 na serikali kwa ajili ya ukarabati. Katika taarifa hiyo ya ujenzi moja ya changamoto iliyotolewa na Mganga wa kituo hicho,  Dk.Hosea Lotto alisema kituo hicho hakina hati miliki.Dk. Lotto alisema pamoja na majengo ya kituo cha afya Hombolo kuwepo toka mwaka 1968,  lakini mpaka hivi sasa  hawana hati miliki kutoka mamlaka husika. Kutok

BREAKING NEWS: NGOMA NI MALI YA AZAM FC, RASMI DILI LIMESHAKAMILIKA, APELEKWA SAUZI

Image
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwa ndani ya jezi ya Azam (kulia) akiwa na kiongozi wa Azam. Uongozi wa Azam FC umethibitisha kuwa umeingia makubaliano ya usajili na mshambuliaji Donald Ngoma, kwa ajili ya msimu ujao 2018/2019. Baada ya kuingia makubaliano hayo, muda wowote kuanzia sasa Azam FC inatarajia kumpeleka mchezaji huyo katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona. Azam FC inaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo kutoka nchini Zimbabwe aliyewahi kuchezea FC Platinum ya huko kabla ya kuhamia Yanga, ni sehemu tu ya mikakati ya benchi la ufundi na uongozi katika kuboresha kikosi kwenye eneo la ushambuliaji kuelekea msimu ujao. Donald Ngoma akiwa Yanga Aidha kama mambo yataenda vizuri, uongozi wa Azam FC unaamini kuwa Ngoma atakuwa ni miongoni mwa nyota wapya wa timu hiyo watakaoonekana kwenye Kombe la Kagame (C

Vyakula Kumi 10 Vya Kuongeza Kinga Ya Mwili

Image
Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni yakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako 1.Yogurt ( Maziwa mtindi ) Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako. 2. Matunda Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, matunda asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda. 3. Vitunguu saumu Hupatikana Kila soko Tanzania! Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI TRA

Image
RAIS John Magufuli amemteua Bi. Khadija Issa Said kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Bima Tanzania (TRA).

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MHE. JAJI MKUU, PROF. IBRAHIM JUMA LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

Image
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiongozana na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) wakielekea katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia)akizungumza na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) alipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) alipomtembelea leo ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) alipomtembelea leo ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Wengine ni wageni Mbali mbali waliokuja kushuhudia jinsi Bunge linavyofanya kazi yake Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akipunga mikono pamoja na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) baada ya kutambulishwa leo ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiwa katika

Lulu Diva aelezea kuhusu kumzalia Rich Mavoko

Image
Muimbaji Lulu Diva amefunguka ukweli wa taarifa za kumzalia mtoto Rich Mavoko mwaka huu. Muimbaji huyo amesema taarifa hizo si za kweli ila anahitaji atapokuwa tayari kufanya hivyo awe na muda wa kutosha tofauti na sasa ambapo muziki umemtinga. “Ni ungo bwana!, nahitaji mtoto wangu ambaye nitazaa apate time yangu na pia baba mtoto awe tayari,” Lulu Diva ameiambia Uhondo, E FM. Alipoulizwa kuhusu kuolewa, alijibu; ‘Soon naolewa lakini bado after miaka mitatu’. Katika hatua nyingine amekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rich Mavoko, huku Mavoko naye akieleza kuwa na mahusiano yake ambayo yamempatia watoto wawili. Lulu Diva na Rich Mavoko kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Ona.

Nape atoa somo kwa Mawaziri

Image
Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye, amewataka Mawaziri katika serikali ya awamu ya tano kuwa na tabia ya kusikiliza ushauri na kukubali kukosolewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Nape amesema hayo leo Mei 25, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kuchangia hoja mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na kuwataka Mawaziri hao kuiga mfano wa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu wake kwani ni watu ambao wanakubali kupokea ushauri. “Wito wangu kwa Mawaziri wengine igeni mfano wa Kalemani, ukiambiwa jambo usilolipenda, wewe ni kiongozi kubali, sikiliza, mimi naamini Kalemani atakwenda vizuri, zipo changamoto kwenye Wizara yako, lakini ninaamini ukiendelea kuwa msikivu yale ambayo yapo juu ya uwezo wako mimi najua watu watakusamehe, lakini yale ambayo yapo ndani ya uwezo wako ukisikiliza na ukayatekeleza tutakuunga mkono” amesema Nape. Mbunge huyo aliendelea kumwaga sifa kwa Waziri Kalemani kwa kufanikiwa kuiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara k