Kijana aliyemuokoa mtoto ghorofani akutana na Rais, apewa uraia na kazi Serikalini
Kijana raia wa nchini Mali, Mamoudou Gassam (22) ambaye Jumamosi
iliyopita amefanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo ambaye
alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, amekutana na Rais wa
Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nzito.
Mamoudou amekutana na Rais Macron mapema Jumatatu hii kwenye Ikulu ya Elysee Palace kwa ajili ya kufanya mazungumzo pamoja na kupongezwa kwa msaada alioutoa.
Rais Macron amempatia cheti cha Uraia wa Ufaransa kijana huyo ambaye alihamia nchini hapo kwa njia zisizokuwa za kihalali takribani miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kutafuta maisha, Lakini pia Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika jeshi la zima moto la Ufaransa.
Kupitia mtandao wa Twitter Rais Macron ameweka picha akiwa Ikulu na kijana Mamoudou na kuandika, “With Mr. GASSAMA who saved Saturday the life of a child climbing 4 floors with bare hands. I announced to him that in recognition of this heroic act he would be regularized as soon as possible, and that the brigade of the firemen of Paris was ready to receive it.”

Comments
Post a Comment