BREAKING NEWS: NGOMA NI MALI YA AZAM FC, RASMI DILI LIMESHAKAMILIKA, APELEKWA SAUZI
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwa ndani ya jezi ya Azam (kulia) akiwa na kiongozi wa Azam.
Uongozi wa Azam FC umethibitisha kuwa umeingia makubaliano ya usajili
na mshambuliaji Donald Ngoma, kwa ajili ya msimu ujao 2018/2019.Baada ya kuingia makubaliano hayo, muda wowote kuanzia sasa Azam FC inatarajia kumpeleka mchezaji huyo katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona.
Azam FC inaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo kutoka nchini Zimbabwe aliyewahi kuchezea FC Platinum ya huko kabla ya kuhamia Yanga, ni sehemu tu ya mikakati ya benchi la ufundi na uongozi katika kuboresha kikosi kwenye eneo la ushambuliaji kuelekea msimu ujao.
Donald Ngoma akiwa Yanga
Tayari mchezaji huyo ameandaliwa jezi namba 11 iliyokuwa ikitumiwa na mshambuliaji Yahaya Mohammed, aliyerejea Aduana Stars ya nchini kwao Ghana.
Tunawaomba mashabiki wetu wa Azam FC wawe watulivu katika kipindi hiki na kuendelea kuisapoti timu, kwani uongozi umejipanga kufanyia kazi ripoti ya benchi ya ufundi na kuboresha kikosi ili kusaka taji la ubingwa msimu ujao.
Comments
Post a Comment