Posts

Mbowe Afunguka Kauli ya Mwisho ya Bilago Kabla ya Kifo

Image
MWENYEKITI wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema maneno ya mwisho aliyoambiwa na aliyekuwa Mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, marehemu Kasuku Bilago kuwa alimwambia anahitaji msaada wa haraka wa matibabu. Akizungumza katika ibada fupi ya kuuaga mwili wa marehemu Bilago, Mbowe amesema wakati alipokuwa nje ya nchi, nchini Afrika Kusini Bilago alimtumia ujumbe kwamba hali yake kiafya si nzuri hivyo anahitaji msaada. “Nilipokuwa safarini nchini Afrika Kusini, mwalimu Bilago aliniambia ninaumwa hivyo naomba ushauri, nikawasiliana na bunge kuhusu taarifa yake ndipo walipomuamishia muhimbilli.Mwalimu aliliona hilo kwamba alikuwa anahitaji msaada wa haraka wa matibabu na kunitumia ujumbe nikiwa Afrika Kusini,” amesema Mbowe. Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa “Ndipo nilifunga safari Ijumaa, Jumamosi nilienda Muhimbili, nilimkuta hali yake imebadilika ghafla akakata kauli, nikaonana na madaktari ili wafanye juhudi za makusudi lakini walijaribu kwa muda wa nusu saa

Mkutano Mkuu wa CCM Mambo Moto

Image
MASIKIO ya wengi yameelekezwa kwenye mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika leo (Jumatatu) na kesho jijini Dar es Salaam, ambapo vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC ) vikitarajiwa kuwasha moto wa uamuzi mgumu unaotajwa kuwa ni nadra kutokea ndani ya chama hicho tawala. Tangu mkutano huo utangazwe ukifuatiwa na kutolewa kwa ripoti ya ya uchunguzi wa mali za CCM nchi nzima kumekuwepo na habari nyingi zinazohusisha uwezekano wa vikao hivyo kutoka na maazimio mazito, hata hivyo, chanzo kutoka ndani ya chama hicho kimeliambia Ijumaa Wikienda kuwa, agenda zake zitaleta mwangwi miongoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla. “Ni vikao vizito vitakavyoamua mambo mazito yenye faida kwa chama chetu, siwezi kusema ni yepi lakini tega masikio utasikia, CCM ni chama kikongwe na makini lazima mikutano yake hasa ya kitaifa iamue mambo makini .“Huwezi kuwa na chama kama hiki, kinachoshika dola halafu kiwe na mikutano ya kitotokitoto, wanaosema kitakuwa moto ni

Kijana aliyemuokoa mtoto ghorofani akutana na Rais, apewa uraia na kazi Serikalini

Image
Kijana raia wa nchini Mali, Mamoudou Gassam (22) ambaye Jumamosi iliyopita amefanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo ambaye alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nzito. Mamoudou amekutana na Rais Macron mapema Jumatatu hii kwenye Ikulu ya Elysee Palace kwa ajili ya kufanya mazungumzo pamoja na kupongezwa kwa msaada alioutoa. Rais Macron amempatia cheti cha Uraia wa Ufaransa kijana huyo ambaye alihamia nchini hapo kwa njia zisizokuwa za kihalali takribani miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kutafuta maisha, Lakini pia Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika jeshi la zima moto la Ufaransa. Kupitia mtandao wa Twitter Rais Macron ameweka picha akiwa Ikulu na kijana Mamoudou na kuandika, “With Mr. GASSAMA who saved Saturday the life of a child climbing 4 floors with bare hands. I announced to him that in recognition of this heroic act he would be regularized as soon as possi

TAJIRI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA, BASTOLA – DAR

Image
MAMLAKA ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewatia mbaroni watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, Ayoub Kiboko na mkewe, Pilli Kiboko, Mei 23, saa 8 usiku wakiwa nyumbani kwao eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam baada ya kuwasaka kwa muda mrefu. Kiboko ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara waliotajwa katika barua za Watanzania waliofungwa Hong Kong, ni maarufu ndani na nje ya nchi na anadaiwa kumiliki hoteli kubwa zaidi ya 10 pamoja nyumba za kifahari katika maeneo mbalimbali hapa jijini. Barua hizo zililetwa nchini Desemba 2014 na Kasisi John Wotherspoon anayesaidia wafungwa katika magereza ya Hong Kong na China na baada ya Watanzania hao kuandika barua hizo wakiwaasa wengine wasifanye biashara hiyo huku wakiwataja wafanyabiashara waliowabebesha dawa hizo za kulevya akiwamo Kiboko. Kamishna wa Operesheni DCEA, Frederick Milanzi alisema katika msako uliofanywa nyumbani kwake usiku wa manane, walimkamata Kiboko akiwa na dawa za kulevya

RATIBA YA SPORTPESA SUPER CUP HII HAPA KUNA ASILIMIA 90 SIMBA NA YANGA KUKUTANA NUSU FAINALI

Image
Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajia kuanza Juni 3 ,2018 kwa timu nane kushirikia ambazo zinadhaminiwa na Kampuni hiyo kubashiri Matokeo Bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda kucheza na Everton nchini Uingereza. Watani wa Jadi Simba na Yanga kuna uwezekano Mkubwa wakakutana Nusu Fainali ya Michuano hiyo huku Derby ya Mashemeji huenda ikatokea tena kama walivyokutana kwenye Fainali ya Msimu uliopita walipocheza uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Ratiba Kamili ni: Robo Fainali 03/06/2018 13:00 Kakamega Home Boys vs Yanga sc 15:15 Gor Mahia vs JKU 04/06/2018 15:00 Kariobangi Sharks vs Simba Sc 05/06/2018 15:00 AFC Leopards vs Singida United Nusu Fainali 07/06/2018 13:00 Winner (Gor Mahia vs JKU) vs (AFC Leorpard s vs Singida Utd) 15:15 Winner (Kakamega Home Boys vs Yanga Sc) vs ( Kariobangi Sharks vs Simba Sc) Mshindi wa tatu 10/06/2018 12:00 Loser Nusu Fainali Fainali 10/06/2018

Waziri Jafo atoa agizo hili

Image
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za  Mitaa (TAMISEMI),  Selemani Jafo, ameagiza  kufikia  mwezi Desemba mwaka huu taasisi zote za serikali katika halmashauri ya  jiji la Dodoma zinatakiwa kupata  hati miliki ya maeneo yao. Aidha,  ametoa muda wa mwezi mmoja kukamilishwa kwa ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo jijini  hapa ambacho kimeonekana kuwa ujenzi wake upo nyuma ikilinganishwa na vituo vingine 208 vinavyokarabatiwa nchini. Jafo alitoa maagizo hayo juzi mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo cha afya Hombolo iliyotolewa na Mganga wa kituo hicho kilichopatiwa fedha kiasi cha Sh. milioni 500 na serikali kwa ajili ya ukarabati. Katika taarifa hiyo ya ujenzi moja ya changamoto iliyotolewa na Mganga wa kituo hicho,  Dk.Hosea Lotto alisema kituo hicho hakina hati miliki.Dk. Lotto alisema pamoja na majengo ya kituo cha afya Hombolo kuwepo toka mwaka 1968,  lakini mpaka hivi sasa  hawana hati miliki kutoka mamlaka husika. Kutok

BREAKING NEWS: NGOMA NI MALI YA AZAM FC, RASMI DILI LIMESHAKAMILIKA, APELEKWA SAUZI

Image
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwa ndani ya jezi ya Azam (kulia) akiwa na kiongozi wa Azam. Uongozi wa Azam FC umethibitisha kuwa umeingia makubaliano ya usajili na mshambuliaji Donald Ngoma, kwa ajili ya msimu ujao 2018/2019. Baada ya kuingia makubaliano hayo, muda wowote kuanzia sasa Azam FC inatarajia kumpeleka mchezaji huyo katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona. Azam FC inaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo kutoka nchini Zimbabwe aliyewahi kuchezea FC Platinum ya huko kabla ya kuhamia Yanga, ni sehemu tu ya mikakati ya benchi la ufundi na uongozi katika kuboresha kikosi kwenye eneo la ushambuliaji kuelekea msimu ujao. Donald Ngoma akiwa Yanga Aidha kama mambo yataenda vizuri, uongozi wa Azam FC unaamini kuwa Ngoma atakuwa ni miongoni mwa nyota wapya wa timu hiyo watakaoonekana kwenye Kombe la Kagame (C

Vyakula Kumi 10 Vya Kuongeza Kinga Ya Mwili

Image
Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni yakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako 1.Yogurt ( Maziwa mtindi ) Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako. 2. Matunda Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, matunda asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda. 3. Vitunguu saumu Hupatikana Kila soko Tanzania! Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI TRA

Image
RAIS John Magufuli amemteua Bi. Khadija Issa Said kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Bima Tanzania (TRA).

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MHE. JAJI MKUU, PROF. IBRAHIM JUMA LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

Image
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiongozana na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) wakielekea katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia)akizungumza na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) alipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) alipomtembelea leo ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) alipomtembelea leo ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Wengine ni wageni Mbali mbali waliokuja kushuhudia jinsi Bunge linavyofanya kazi yake Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akipunga mikono pamoja na Mhe. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma (kushoto) baada ya kutambulishwa leo ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiwa katika

Lulu Diva aelezea kuhusu kumzalia Rich Mavoko

Image
Muimbaji Lulu Diva amefunguka ukweli wa taarifa za kumzalia mtoto Rich Mavoko mwaka huu. Muimbaji huyo amesema taarifa hizo si za kweli ila anahitaji atapokuwa tayari kufanya hivyo awe na muda wa kutosha tofauti na sasa ambapo muziki umemtinga. “Ni ungo bwana!, nahitaji mtoto wangu ambaye nitazaa apate time yangu na pia baba mtoto awe tayari,” Lulu Diva ameiambia Uhondo, E FM. Alipoulizwa kuhusu kuolewa, alijibu; ‘Soon naolewa lakini bado after miaka mitatu’. Katika hatua nyingine amekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rich Mavoko, huku Mavoko naye akieleza kuwa na mahusiano yake ambayo yamempatia watoto wawili. Lulu Diva na Rich Mavoko kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Ona.

Nape atoa somo kwa Mawaziri

Image
Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye, amewataka Mawaziri katika serikali ya awamu ya tano kuwa na tabia ya kusikiliza ushauri na kukubali kukosolewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Nape amesema hayo leo Mei 25, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kuchangia hoja mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na kuwataka Mawaziri hao kuiga mfano wa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu wake kwani ni watu ambao wanakubali kupokea ushauri. “Wito wangu kwa Mawaziri wengine igeni mfano wa Kalemani, ukiambiwa jambo usilolipenda, wewe ni kiongozi kubali, sikiliza, mimi naamini Kalemani atakwenda vizuri, zipo changamoto kwenye Wizara yako, lakini ninaamini ukiendelea kuwa msikivu yale ambayo yapo juu ya uwezo wako mimi najua watu watakusamehe, lakini yale ambayo yapo ndani ya uwezo wako ukisikiliza na ukayatekeleza tutakuunga mkono” amesema Nape. Mbunge huyo aliendelea kumwaga sifa kwa Waziri Kalemani kwa kufanikiwa kuiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara k

Mkapa, Mangula, Mwenyekiti UVCCM Wamtembelea Magufuli Ikulu – Pichaz

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kushoto) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli akijadiliana jambo na mzee Mkapa (kulia) pamoja na Mangula (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mndolwa, Kabaka pamoja na Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Magufuli akiagana na Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati

Zipitie Nafasi Za Kazi 31 Kutoka REA, Mwisho wa Kuomba June 20, 2018

Image
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA   PRESIDENT’S OFFICE PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT Ref.No.EA.7/96/01/J/134 23rd May, 2018 VACANCIES ANNOUNCEMENT  On behalf of Rural Energy Agency (REA), President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 31 vacant posts as mentioned below; 1.0 INTRODUCTION:  RURAL ENERGY AGENCY (REA) Rural Energy Agency (REA) is an Autonomous Body under the Ministry of Energy and Minerals of the United Republic of Tanzania. Its main role is to promote and facilitate improved access to modern energy services in rural areas of Mainland Tanzania. REA became operational in October 2007. REA Vision: Transformation of rural livelihoods through provision of modern energy services. REA Mission: To promote and facilitate availability and access to modern energy services in rural Mainland Tanzania. 1.1 DIRECTOR OF HUMAN RESOURCE AND ADMINISTRATION (1 POST) (RE-ADVERTISED) – 1 POST  1.2 REPORTS TO: DIRE

‘Vita’ ya Alikiba na Samatta Imefika Pabaya

Image
NAHODHA wa Timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars na Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta ameingia kwenye vita ya ki-sport na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba inayotarajiwa kufanyika Juni 9, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu katika mashule. Samatta amesema mechi hiyo itakuwa itamuhusisha yeye na marafiki zake dhidi ya Alikiba na marafiki zake pia. “Itakuwa mechi ya hisani kama zilizo nyingine ambazo zimekuwa zikifanywa na wachezaji wakubwa, hii ni kati ya Samatta 11 na Alikiba 11, nitachagua marafiki zangu na Kiba atachagua marafiki zake. Nataka nifanye moja lakini itakuwa na radha tofauti, kwani timu pinzani itakuwa ya Alikiba. “Ok, nimepewa jukumu la kuandaa jeshi la maangamizi mchezaji gani ungependa kumuona siku iyo awe wa sasa au wa zamani?” amesema Samatta. Alikiba amesema amefurahi urafiki wake na Samatta kuzalisha kitu hicho kizuri huku akiwaomba wapenzi n

DKT ABBASI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO IMARISHENI USHIRIKIANO NA WATENDAJI WA KADA TOFAUTI KUTANGAZA MAFANIKIO YA SERIKALI

Image
MAAFISA Habari na Mawasiliano Serikalini  wametakiwa kujenga timu ya ushirikiano wa pamoja na Wataalamu wa kada mbalimbali waliopo katika maeneo yao ya kazi ili kutangaza vyema mafanikio ya miradi na program zilizotekelezwa na zinazotekelezwa na Serikali. Hayo yamesemwa jana Mkoani Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya siku tano ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali za Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Dkt. Abbasi alisema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa watendaji wote wa Serikali wanakuwa mstari wa mbele katika kuwaletea maendeleo ya haraka  wananchi wake kwani Serikali inajenga nyumba moja, hivyo ni wajibu wa watumishi wote kuungana pamoja katika kusukuma mbele gurudumu hilo hususani katika maeneo ya Mikoa na Halmashauri ambapo Serikali hupeleka kiasi kikubwa