DKT ABBASI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO IMARISHENI USHIRIKIANO NA WATENDAJI WA KADA TOFAUTI KUTANGAZA MAFANIKIO YA SERIKALI
MAAFISA Habari na Mawasiliano
Serikalini wametakiwa kujenga timu ya ushirikiano wa pamoja na
Wataalamu wa kada mbalimbali waliopo katika maeneo yao ya kazi ili
kutangaza vyema mafanikio ya miradi na program zilizotekelezwa na
zinazotekelezwa na Serikali.
Hayo yamesemwa jana Mkoani
Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya siku
tano ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Vitengo vya Habari na
Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali za Mikoa
ya Arusha na Kilimanjaro.
Dkt. Abbasi alisema malengo ya
Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa watendaji wote wa Serikali
wanakuwa mstari wa mbele katika kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi
wake kwani Serikali inajenga nyumba moja, hivyo ni wajibu wa watumishi
wote kuungana pamoja katika kusukuma mbele gurudumu hilo hususani katika
maeneo ya Mikoa na Halmashauri ambapo Serikali hupeleka kiasi kikubwa
cha pesa za miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha Christopher Kazeri (katikati)
akizungumza na Uongozi wa Chama cha Maafisa Habari Serikalini (TAGCO) na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi wakati wa
ziara yao ya kutembelea Kitengo vya Habari na Mawasiliano Serikali
katika Halmashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.
“Katika Serikali ya Awamu ya Tano,
ukiwa Afisa Mifugo, Nyuki, Maliasili, Tehama na wengineo tunawajibika
kushirikiana kwa karibu zaidi na Maafisa Habari na Mawasiliano kwa kuwa
shughuli zao zinahusu maendeleo ya wananchi, hivyo ni wajibu wa taarifa
zao ziwafikie wananchi kwa wakati ili kuweza kujibu hoja na kutoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali” alisema Dkt. Abbasi.
Aidha Dkt. Abbasi alisema Serikali
tayari imetoa maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Mikoa na Halmashauri
zote nchini kuhakikisha kuwa Maafisa Habari na Mawasiliano
wanashirikishwa kwa karibu zaidi katika kupata taarifa mbalimbali za
maeneo yao ya kazi ikiwemo kushiriki katika vikao vya juu vya maamuzi
katika Mikoa, Halmashauri, Wizara, Taaasisi na Wakala.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema
Maafisa Habari Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka ya Serikali
za Mitaa wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutengeneza majukwaa
mbalimbali ya utoaji wa taarifa zao kwa umma ikiwemo matumizi ya
mitandao ya kijamii kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kujibu hoja za
kwa wanaopinga maendeleo yanayofikiwa na Serikali kwa wananchi wake.
Katibu wa Chama cha Maafisa Habari
na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Abdul Njaidi katikati akichangia
hoja wakati wa mkutano baina ya TAGCO na Ofisi ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru iliyolenga kujionea utendaji kazi wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmnashauri hiyo jana
Jumatano Mei 23, 2018.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha, Christopher Kazeri alisema
Halmashauri hiyo imefanya jitihada mbalimbali za kujenga ushirikiano
baina ya Wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo na Kitengo cha Habari na
Mawasiliano hususani katika kuratibu shughuli za utoaji wa taarifa
mbalimbali za matukio katika Halmashauri hiyo.
“Kwa sasa Afisa Habari wetu
anashiriki katika kikao chetu cha juu cha kila mwezi katika Halmashauri
ambacho kinaelezea utekelezaji wa miradi, kazi na majukumu mbalimbali,
ambapo kwa kufanya hivyo tumeweza kufanya vizuri katika uwekaji wa
taarifa sahihi na za wakati katika tovuti yetu ya Halmashauri” alisema
Kazeri.
Aidha Kazeri alisema Ofisi yake
pia imepanga kuweka mipango na mikakati mbalimbali ya kuimarisha kitengo
cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri hiyo kwa kuhakikisha kuwa
watendaji wake wanapata mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuwajengea
uwezo wa kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akichangia hoja wakati
wakati wa mkutano baina ya TAGCO, Idara ya Habari (MAELEZO) na Ofisi ya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru iliyolenga kujionea utendaji
kazi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmnashauri hiyo
jana Jumatano Mei 23, 2018.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Paschal Shelutete malengo ya ziara hiyo ni kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali na hivyo kuweza kuwa na mikakati iliyo bora zaidi katika kuisemea na kutangaza mafanikio ya Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Paschal Shelutete malengo ya ziara hiyo ni kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali na hivyo kuweza kuwa na mikakati iliyo bora zaidi katika kuisemea na kutangaza mafanikio ya Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri akifurahia jambo na Mkurugenzi wa
Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Mjumbe wa TAGCO,
Innocent Byarugaba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliolenga
kujionea utendaji kazi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika
Halmnashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri (wa tatu kushoto) akiwa katika
picha ya pamoja na Uongozi wa TAGCO wakiongozwa na Mwenyekiti wao,
Paschal Shelutete mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao
uliofanyika jana Mei 23, 2018 kwa ajili ya kujionea utendaji kazi wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmashauri hiyo.
Aliongeza kuwa TAGCO kwa kushiriana na Idara ya Habari (MAELEZO) imekusudia kufanya ziara hiyo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wote nchini ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uelewa wa pamoja katika kuwa na njia na namna bora zaidi ya kubuni mikakati ya kuisemea Serikali.
Aliongeza kuwa TAGCO kwa kushiriana na Idara ya Habari (MAELEZO) imekusudia kufanya ziara hiyo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wote nchini ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uelewa wa pamoja katika kuwa na njia na namna bora zaidi ya kubuni mikakati ya kuisemea Serikali.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri (katikati) akibadilishana mawazo na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Uongozi
wa Chama cha Maafisa Serikali (TAGCO), mara baada ya kumalizika kwa
mkutano baina yao jana Mei 23, 2018 uliolenga kujoinea utendaji kazi wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalimni katika Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akiongoza kikao cha pamoja na Watendaji wa
Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Maafisa
Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha wakati wa ziara
ya pamoja iliyoratibiwa na TAGCO Kwa ajili ya kujonea utendaji kazi wa
Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri hiyo jana Jumatano
Mei 23, 2018.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro Yohana Sintoo (katikati) akizungumza
na Watendaji wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikali pamoja
na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi (wa
kwanza kushoto) wakati walipofika Ofisini kwake kujionea utendaji kazi
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri hiyo jana
Jumatano Mei 23, 2018.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus (kulia) akibadilishana mawazo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro
Yohana Sintoo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao hapo jana Mei 23,
2018 baina ya TAGCO kwa pamoja na Idara ya Habari (MAELEZO) wakiongozwa
na Mkurugenzi wa Idara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi (katikati).
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Paschal Shelutete akizungumza
katika mahojiano ya kipindi maalum cha Redio Boma FM ya Wilayani Hai
Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya TAGCO na Idara ya Habari (MAELEZO)
kujiounea utendaji kazi wa Kitendo cha Habari na Mawasiliano katika
Halmashauri hiyo jana Mei 23, 2018. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Dkt Hassan Abbasi.
(NA MPIGAPICHA WETU
…………………
Na Mwandishi Wetu
MAELEZO
ARUSHA
24.5.2018
Comments
Post a Comment