Posts

Breaking News: Mahakama Yaamuru Hans Pope na Lauwo Wakamatwe

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo April 30, 2018 imetoa amri kwamba Mwenyekiti wa Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani ili kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’. Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao. Wakili Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao tangu Machi mwaka huu bila mafanikio hivyo akaomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, nyaraka na kutakatisha fedha kiasi cha Dola za Marekani 300,000.

Chadema Wakanusha Lissu Kuerejea Nchini

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mapema Januari mwaka huu. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene amesema; Kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za kwamba Lissu anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia juzi na kwamba amemaliza matibabu yake kitu ambacho si cha kweli na kimezua taharuki. Makene amesema, Lissu hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote kuhusu kurejea kwake hapa chini kwa sababu  hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwishoni wiki hii au wiki ijayo. Chadema kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata Lissu wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo. Lissu yupo nchini Ubelgi

Makonda Ampokea Ahmed Aliyepooza Akitokea China

Image
Ahmed alikwenda nchini China miezi miwili iliyopita ambapo hali yake inaendelea vizuri  baada ya kupatiwa matibabu. Kijana huyo alipata tatizo hilo la kupooza baada ya kuumia wakati akifanya mazoezi ya kuogelea. Ahmed Albaiti akiwasili uwanja wa ndege Dar es Salaam akitoka katika matibabu nchini China leo. Picha na Denis Mtima | GPL

RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma wa pili kutoka kulia wakivuta utepe kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Sherehe hizo za ufunguzi zilifanyika katika kijiji cha Ndolela kilichopo Isimani nje kidogo ya mji wa Iringa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu Yoshida wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wageni k

Serengeti Boys wanyakua ubingwa wa CECAFA U- 17

Image
Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imeibuka na ubingwa wa CECAFA U-17 baada ya kuifunga timu ya vijana ya Somalia mabao 2-0 katika fainali iliyopigwa huko Burundi. Serengeti Boys imecheza vizuri mchezo huo wa fainali na kufanikiwa kuongoza kwa bao moja hadi mapumziko kabla ya kuongeza bao la pili kipindi cha pili na kujihakikishia ubingwa huo. Mabingwa hao wapya wa Afrika Mashariki na Kati, wamekabidhiwa kombe hilo na mgeni rasmi wa fainali hiyo ambaye ni Rais wa shirikisho la soka barani Africa Ahmed Ahmed. Vijana hao wametinga fainali hiyo baada ya kuwatoa timu ya Taifa ya Kenya U17 kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Alhamisi. Wakati Somalia imeingia fainali kwa kuifunga Uganda 1-0. Moja ya timu zilizofungwa na vijana hao katika hatua ya makundi ni pamoja na Sudan na Uganda. Katika michuano hii timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar (Karume Boys) iliondolewa kutoka na kuwa na wachezaji we

ALIKIBA NA MKEWE AMINA WALIVYOINGIA UKUMBINI

Image
STAA wa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ na mkewe, Amina raia wa Kenya wameingia katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena uliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea harusi yao usiku huu wa Aprili 29, 2018. Katika sherehe hizo ambazo pia zinahusisha harusi ya mdogo wake Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde. Tazama picha hizi. Picha na Azam TV.

ABDU KIBA NA MKEWE WALIVYOINGIA UKUMBINI

Image
MKALI wa Bongo Fleva, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda tayari wameshaingia katika Ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea harusi yao usiku huu. Katika sherehe hizo ambazo pia zinahusisha harusi ya Alikiba na mkewe, Amina imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde. Tazama picha hizi. Picha na Azam TV.

MAMA KIKWETE, UMMY MWALIMU WATINGA HARUSI YA KIBA

Image
MKE wa Rais wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepata fursa ya kuhudhuria katika harusi ya staa wa Bongo Fleva, Alikiba na mkewe, Amina katika ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam usiku huu wa Aprili 29, 2018. Mama Salma ambaye pia ni mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto, Wanawake, Jinsia na Wazee, Dkt. Ummy Mwalimu katika seherehe hiyo. Katika sherehe hiyo pia inahusisha harusi ya mdogo wa Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda ambao walifunga ndoa Jumapili iliyopita. Viongozi wengine waliopata fursa ya kuhudhuria sherehe hiyo ni Naibu Waziri wa Kazi ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (kulia), na Mwenyekiti wa UVCCM, Khery James (kushoto). Picha na Azama TV.

WAMILIKI SOBA HOUSE WAWAJIBU WABUNGE TUHUMA ZA KUWACHOMA SINDANO WAATHIRIKA DAWA ZA KULEVYA

Image
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki wa Sober House Tanzania, Pili Missanah (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Baadhi ya viongozi wa  Sober House Tanzania walioshiriki mkutano huo na waandishi wa habari. WAMILIKI wa nyumba zinazosaidia waathirika kujinusuru na dawa za kulevya nchini maarufu kama Soba house wamejibu tuhuma za kuwachoma vijana sindano pindi wapatapo nafuu. Akiongea na waandishi wa habari leo Jiji Dar es Salaam Katibu wa Umoja wa Soba house nchini, Pili Missanah ambaye ni mmoja wa wamiliki wa vituo hivyo ameeleza kuwa, April 25 mwaka huu katika mjadala wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baadhi ya wabunge walieleza kuhusu tabia chafu  za baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo kuwachoma sindano za dawa za kulevya baadhi ya waathirika pindi wanapokaribia kupona ili wazazi au walezi waendelee kuchangia fedha kwenye nyumba hizo. Pili ameeleza kuwa lengo la nyumba hizo sio baya bali ni kuwasaidia waathirika wa dawa za k

FT: SIMBA 1-0 YANGA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA (KADI NYEKUNDU KESSY)

Image
MPIRA UMEKWISHA DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 90 Yanga wanaingia lakini Simba wamejaa nyum SUB Dk 83, Simba wanamtoa Gyan nafasi yake inachukuliwa na Paul  Bukaba Dk 82, Mahadhi anaingia na kujaribu kupiga krosi, Mkude ameunawa ni faulo si mbali na lango la Simba Dk 76, krosi maridadi katika lango la Simba, Chirwa anaruka na kupiga kichwa lakini ni goal kick Dk 70 Kichuya anapangua watu wawili, anatoa pasi kwa Bocco, naye anampa Kapombe kona ya saba ya Simba, Yanga hawana kona hata moja Dk 70 sasa, bado inaonekana Yanga wanafanya mashambulizi ya kufunga, lakini Simba wanapoteza nafasi nyingi na lazima wazitumie mapema maana Yanga bado nao wana uwezo wa kufunga Dk 67, Kichuya anamtoka Makapu, anaingia na kupiga krosi safi kabisa, Dante anapiga kichwa na kuokoa Dk 65 Yanga wanaonekana wanaanza kufunguka lakini Mlipili yuko makini, anaokoa unakuwa wa kurushwa Dk 63 mpira wa Okwi unaokolewa na kuwa kona ya sita ya SImba, inachongwa na kuokolewa SUB Dk 62, Yanga inafanya sub

HAIJAWAHI KUTOKEA: Kim Jong-un Avuka Mpaka wa Kijeshi, Aingia Korea Kusini

Image
KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kuvuka mstari wa kijeshi uliowekwa kuyagawa mataifa ya Korea tangu vita vya Korea vya mwaka 1950-1953, ambapo ameingia Korea Kusini na kukutana na Rais wa nchi hiyo, ambaye amekuwa hasimu wake kwa muda mrefu, Moon Jae-in. , Tukio hilo la kihistoria limetokea leo Aprili 27, 2018 ambapo tukio hilo lilishangiliwa kwa mbwembwe na viongozi wa Korea Kusini na mwenzao wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa kushikana mikono katika mpaka huo kabla ya kukaribishwa na kuingia nchini humo. Hata hivyo shughuli zote za taifa la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili na baadaye watu walishangaa baada ya Kim kumualika kiongozi wa Korea Kaskazini kuvuka kwa muda mfupi katika mstari wa mpaka wa mataifa hayo mawili kuingia Korea Kaskazini, kabla ya wawili hao kurudi tena Korea Kusini muda wote huo wakiwa wameshi

RAIS ZUMA KUOA MKE WA 7, NI BINTI WA MIAKA 24 ALIYEZAA NAYE

Image
ALIYEKUWA Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameushangaza umma baada ya kuwepo na taarifa za kutarajia kuoa mke wa saba, binti mdogo mwenye umri wa miaka 24. Taarifa hizo zimethibitishwa na binti huyo anayetarajiwa kuolewa na Zuma, Nonkanyiso Conco, kupitia chombo cha habari cha Times Live nchini humo. “Ndio tunaoana, hayo ndiyo naweza kusema kwa sasa, nahitaji kutoa taarifa kabla sijafanya interview (mahojiano) yoyote”, amesikika binti huyo akiuambia mtandao wa Times Live. Conco inti huyo tayari ana mtoto mchanga aliyezaa na Jacob Zuma siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Zuma, April 12, na tayari mahali imeshatolewa. Zuma ambaye ana miaka 76 mpaka sasa ameshaoa mara sita, na hii itakuwa ni mara ya saba kufunga ndoa, Tukio hilo limeonekana kuwakera baadhi ya wananchi wa Afrika Kusini na kutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, wakisema binti huyo ni mdogo sana kwa Zuma, kwani wana tofauti ya miaka 52.

Siri Wema Kuutosa Msiba wa Masogange Yafichuka!

Image
Wema Sepetu BAADA ya kuwa gumzo msibani wakati wa kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa video queen kwenye nyimbo mbalimbali za Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange’ kutokana na kutoonekana, siri imefichuka ya msanii wa filamu, Wema Sepetu kuutosa msiba huo. Awali habari zilidai kwamba Wema alishindwa kuhudhuria kwenye msiba huo kutokana na kwamba yeye na marehemu Masogange walikuwa na bifu kali na hawakuwahi kupatana. “Unajua Wema na Masogange walikuwa hawaivi, sasa inawezekana ndiyo maana hajaonekana msibani. Au ana sababu nyingine? Mimi kwa kweli nimeshangaa kutomuona,” alisikika akisema mmoja wa waombolezaji aliyekuwa amefika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar kuuaga mwili wa Masogange. SIRI YAFICHUKA Kutokana na gumzo la Wema kuutosa msiba huo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini iliita bila kupokelewa. Baada ya kutopokelewa, gazeti hili liliamua kumtafuta meneja wake, Neema Ndepanya ambaye alitoa siri ya Wema kutohudhuria m

Makaburi ya Vigae si Salama

Image
TAARIFA za watafiti zimeeleza kuwa matumizi ya maru maru (tiles, marble, terrazzo) katika kujengengea makaburi siyo salama kwa ardhi, kwani yana kemikali kali ambayo inaathiri udongo. Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa Sayansi ya Mazingira na Kilimo, Prof. Julius Zake kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda , katika ripoti yake ya udongo wa Uganda huku akieelza njia sahihi ya kutumia mbolea na kueleza kwamba ujenzi wa makaburi kwa tiles unaongeza hatari kubwa ya udongo kushindwa kuzalisha. “Zamani watu walikuwa wanatumia nguo maalum (backcloth ) kuzikia wapendwa wao, sasa hivi watu wanakufa sana na wanazikwa kila mahali kwa wingi,tiles haziwezi kuharibika zinaingiliana na mizizi inayorutubisha udongo na kusaidia uzalishaji, hivyo udongo unaathirika na kemikali”, amesema mwanasayansi huyo. Mtaalamu huyo amesema ardhi sasa hivi imekuwa na acid nyingi na kusabaisha kushindwa kuwa na rutuba, ya kuweza kustawisha mazao na kutunza mazingira. CRE

Dodoma yapiga marufuku nyama ya nguruwe

Image
WAKATI leo mkoa wa Dodoma ukiwa mwenyeji wa maadhimisho ya sikuku ya Muungano halmashauri ya manispaa ya Dodoma imepiga marufuku biashara ya nyama ya nguruwe pamoja na mazao yake kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe. Kwamijibu wa taarifa iliyotolewa na Daktari wa mifugo manispaa ya Dodoma Dk, Innocent Kimweri jana alisema kuwa kwa mamalaka aliyopewa na kifungu namba 17 cha sheria ya magonjwa ya mifugo namba 17 ya mwaka 2003 anatangaza kuwa hivi sasa manispaa ya Dodoma inamlipuko wa homa ya nguruwe. Alisema kutokana na hali hiyo kuanzia sasa anaweka zuio la biashara ya nguruwe pamoja na mazao yake hadi hapo itakapo tangazwa vinginevyo. “Hakuna mnyama yeyote wa jamii ya Nguruwe, ngiri nguruwe pori au nguruwe wa kufungwa atakaye ruhusiwa kuingia au kutoka nje ya wilaya ya Dodoma pasipo ruhusa ya maandishi kutoka kwa daktari wa mifugo wa wilaya ya Dodoma mjini”alisema Dk, Kimweri Vilevile alisema kuwa hakuna bidhaa inayotokana na nguruwe ikiwemo m

MSIBA WA MASOGANGE WAZIMA NDOA YA ABDU KIBA

Image
MSIBA wa aliyekuwa video queen mkali Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ aliyefariki Ijumaa iliyopita, umezima tukio kubwa la kufunga ndoa la msanii wa Bongo Fleva, Abdul Kiba ambaye alioa jana alfajiri. Abdul Kiba ambaye amefunga ndoa siku tatu tu baada ya kaka yake, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ aliyemuoa Amina Khaleef huko Mombasa nchini Kenya. Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake ya Jeraha alifunga ndoa hiyo jijini Dar, jana kwenye Msikiti wa Kichangani, Magomeni ambapo alimuoa mchumba wake wa muda mrefu, Luwada Hassan. Habari zilizolifikia Ijumaa Wikienda jana zilieleza kuwa, huenda Ali Kiba na Abdul Kiba wakafanya sherehe ya pamoja ya harusi Aprili 29, mwaka huu kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi la wao kufunga ndoa. Taarifa zilieleza kuwa, baada ya Ali Kiba na Abdul Kiba kuoa, dada yao, Zabibu Kiba, naye anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na beki za zamani wa Timu ya Simba ambaye kwa sasa an

RC GAMBO AONGOZA MAZISHI YA LEYLA ARUSHA

Image
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo , leo ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Leyla aliyeuawa na mumewe kwa kuchomwa visu na mumewe huko Uingereza wiki kadhaa zilizopita. Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha. Kaburi la marehemu Leyla likiwekwa sawa baada ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha leo. Mwili wa marehemu Leyla aliyeuawa na mumewe kwa kuchomwa visu na mumewe huko Uingereza wiki kadhaa zilizopita ukipelekwa makaburini. Mazishi yakiendelea. (Habari na Korumba Moshi, Arusha)