RAIS ZUMA KUOA MKE WA 7, NI BINTI WA MIAKA 24 ALIYEZAA NAYE

ALIYEKUWA Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameushangaza umma baada ya kuwepo na taarifa za kutarajia kuoa mke wa saba, binti mdogo mwenye umri wa miaka 24.
Taarifa hizo zimethibitishwa na binti huyo anayetarajiwa kuolewa na Zuma, Nonkanyiso Conco, kupitia chombo cha habari cha Times Live nchini humo. “Ndio tunaoana, hayo ndiyo naweza kusema kwa sasa, nahitaji kutoa taarifa kabla sijafanya interview (mahojiano) yoyote”, amesikika binti huyo akiuambia mtandao wa Times Live.

Conco inti huyo tayari ana mtoto mchanga aliyezaa na Jacob Zuma siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Zuma, April 12, na tayari mahali imeshatolewa. Zuma ambaye ana miaka 76 mpaka sasa ameshaoa mara sita, na hii itakuwa ni mara ya saba kufunga ndoa,
Tukio hilo limeonekana kuwakera baadhi ya wananchi wa Afrika Kusini na kutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, wakisema binti huyo ni mdogo sana kwa Zuma, kwani wana tofauti ya miaka 52.

Comments

Popular posts from this blog