Breaking News: Mahakama Yaamuru Hans Pope na Lauwo Wakamatwe

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo April 30, 2018 imetoa amri kwamba Mwenyekiti wa Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani ili kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao. Wakili Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao tangu Machi mwaka huu bila mafanikio hivyo akaomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, nyaraka na kutakatisha fedha kiasi cha Dola za Marekani 300,000.

Comments

Popular posts from this blog