FT: SIMBA 1-0 YANGA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA (KADI NYEKUNDU KESSY)
MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90 Yanga wanaingia lakini Simba wamejaa nyum
SUB Dk 83, Simba wanamtoa Gyan nafasi yake inachukuliwa na Paul Bukaba
Dk 82, Mahadhi anaingia na kujaribu kupiga krosi, Mkude ameunawa ni faulo si mbali na lango la Simba
Dk 76, krosi maridadi katika lango la Simba, Chirwa anaruka na kupiga kichwa lakini ni goal kick
Dk 70 Kichuya anapangua watu wawili, anatoa pasi kwa Bocco, naye anampa Kapombe kona ya saba ya Simba, Yanga hawana kona hata moja
Dk 70 sasa, bado inaonekana Yanga wanafanya mashambulizi ya kufunga, lakini Simba wanapoteza nafasi nyingi na lazima wazitumie mapema maana Yanga bado nao wana uwezo wa kufunga
Dk 67, Kichuya anamtoka Makapu, anaingia na kupiga krosi safi kabisa, Dante anapiga kichwa na kuokoa
Dk 65 Yanga wanaonekana wanaanza kufunguka lakini Mlipili yuko makini, anaokoa unakuwa wa kurushwa
Dk 63 mpira wa Okwi unaokolewa na kuwa kona ya sita ya SImba, inachongwa na kuokolewa
SUB Dk 62, Yanga inafanya sub ya pili, Pius Buswita anaingia kuchukua nafasi ya AjibDk 62, Mahadhi anamuweka Kichuya chini, nje kidogo ya msitari wa 18
Dk 61 mpira wa adhabu wa Ajibu unatoka nje na kuwa goal kick. Mwamuzi anakuwa mkali kwa Manula ambaye anaonekana kama anataka kupoteza muda hivi
Dk 59 Okwi anagongeana faulo na Kichuya lakini inakuwa ya kizembe na Yanga wanafanya kazi nzuri ya kuokoa, mwisho offside
Dk 58 Tshishimbi anamshika Okwi na kumuweka chini, mwamuzi anasema faulo
Dk 58 mpira wa kona ya tano ya Simba, Mkude anaachia mkwaju mkuuuubwaaaa
KADI NYEKUNDU Dk 48, Kessy analambwa kadi ya njano ya pili na kuandika nyekundu, ilikuwa ni baada ya kumuangusha Kwasi
Dk 47, Mahadhi anaingia vizuri kabisa, krosi nzuri lakini Manula yuko makini, anadaka
Dk 45 mpira umeanza kwa kasi na Bocco anagongwa na Yondani na sasa yuko chini, kuna mzozo pale unaendelea
SUB Dk 45, Yanga wanafanya mabadiliko ya kwanza kwa kumuingiza Juma Mahadhi kuchukua nafasi ya Rapharl Daud
MAPUMZIKO
-Okwi anamtoka Dante na kuachia krosi safi kabisa, Yondani anaokoa
-Mhilu anaingia anathibitiwa
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45 Yanga wanacheza kama vile waji mbele maana wanakwenda taratibu na zaidi wanacheza katika eneo lao
Dk 44 pasi nzuri Okwi ndani ya boksi la Yanga, anakwenda chini na mwamuzi anasema mwanamume kugangamala, twende
KADI Dk 39, kadi ya kwanza ya njano inakwenda kwa Kessy baada ya kuonyesha uababe
GOOOOOOOOOO Dk 37, mpira wa adhabu wa Kichuya, Erasto Nyoni anatupia mpira wavuni na kuandika bao la kwanza kwa Simba
Dk 34 sasa, Kichuya alikuwa chini, ameishaamka na Yondani anamuweka chini Kapombe, faulo, itapigwa na Kichuya
Dk 34 sasa, Kichuya alikuwa chini, ameishaamka na Yondani anamuweka chini Kapombe, faulo
Dk 32, Simba wanagongeana vizuri lakini Yanga wanaonyesha umahiri tena katika kuondosha hatari
Dk 30 sasa, kipa Manula yuko chini pale akipatiwa matibabu, inaonekana aliumia alipokwenda kuokoa mpira
Dk 28 Simba wanamsahau Chirwa, Mhilu anapiga krosi maridadi lakini Manula anadaka vizuri
Dk 23 kona inachongwa na Kapombe, inatua kichwani mwa Okwi, mpira unatoka sentimeta chache nje ya lango la Yanga. Goal kick
Dk 22 Okwi anaingia tena, mpira unaokolewa na kuwa kona nyingine. Ni kona ya tatu kwa Simba, inaokolea na kuwa kona ya nne ya Simba
Dk 21, mpira wa kuchonga wa Kichuya kidogo uingie nyavuni lakini Rostand anadaka kwa umakini mkubwa
Dk 18, Kichuya anachonga kona nzuri kabisa, inaokolewa na kuwa kona tena, anaichonga tena, inaokolewa
Dk 17 inakatika, si pambano lenye mvuto sana, kila upande unasikilizia sana na faulo ndogondogo zimekuwa nyingi sana
Dk 14, krosi ya Kwasi ndani ya lango la Yanga lakini Gyan anamsukuma Ajibu, faulo
Dk 13 ukiangalia mchezo umekuwa hauna ladha sana kwa kuwa kila upande uko makini sana na unavizia
Dk 10, Okwi anawatoka mabekiwa Yanga lakini anazuiliwa vizuri kabisa na Yondani
Dk 8, Manula analazimika kutoka nje ya 18 na kupiga mpira kichwa ili kuuondoa na kumuwahi Chirwa aliyekuwa katika kasi
Dk 7 bado game inaonekana haijatulia na hakuna mashambulizi makali na badala yake mpira unachezwa katikati zaidi
Dk 6, mpira bado unachezwa katika ya uwanja, Simba wakiwa wamerudi nyuma kidogo na Yanga wanamiliki zaidi mpira
Dk 4, Okwi alimsukuma Rostand wakati akipiga mpira, ameishaamka na mpira unaendelea
Dk 4, Ajibu anamweka chini Gyan, mwamuzi anasema ni faulo naye anasema hakufanya madhambi
DK 2, Ajibu anageuka vizuri na kuachia mkwaju lakini manula yuko vizuri
Dk 1 Simba nao wanaingia kwenye kasi lango la Yanga lakini pasi ya Kichuya inazuiliwa vizuri na Gadiel
Dk 1, mechi inaanza na Yanga ndiyo wanaanza kusukuma gozi kuelekeza upande wa Simba
MWAMUZI:
Mwamuzi ni Emmanuel Mwandembwa, ana umri wa miaka 34
Comments
Post a Comment