HAIJAWAHI KUTOKEA: Kim Jong-un Avuka Mpaka wa Kijeshi, Aingia Korea Kusini


KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kuvuka mstari wa kijeshi uliowekwa kuyagawa mataifa ya Korea tangu vita vya Korea vya mwaka 1950-1953, ambapo ameingia Korea Kusini na kukutana na Rais wa nchi hiyo, ambaye amekuwa hasimu wake kwa muda mrefu, Moon Jae-in.

,

Tukio hilo la kihistoria limetokea leo Aprili 27, 2018 ambapo tukio hilo lilishangiliwa kwa mbwembwe na viongozi wa Korea Kusini na mwenzao wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa kushikana mikono katika mpaka huo kabla ya kukaribishwa na kuingia nchini humo.




Hata hivyo shughuli zote za taifa la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili na baadaye watu walishangaa baada ya Kim kumualika kiongozi wa Korea Kaskazini kuvuka kwa muda mfupi katika mstari wa mpaka wa mataifa hayo mawili kuingia Korea Kaskazini, kabla ya wawili hao kurudi tena Korea Kusini muda wote huo wakiwa wameshikana mikono.



Viongozi hao walikagua gwaride ambalo likikuwa limevalia nguo za kitamaduni upande wa Korea Kusini ambapo wawili hao na baadaye walielekea katika jumba la amani huko Panmunjom, eneo la kijeshi katika mpaka huo ili kuanza mazungumzo yao.



Kim alisema kuwa anaamini kutakuwa na mazungumzo yenye mafanikio ambapo mkutano huo wa kihistoria utaangazia masuala ya silaha za kinyuklia na uwezekano wa makubaliano ya amani.
Mengi yatakayozungumzwa ni mambo ambayo tayari yameafikiwa awali lakini wachambuzi wengi bado wana wasiwasi kuhusu uaminifu wa Korea Kaskazini katika makubaliano hayo hasa kuacha shughuli ya utengezaji wa silaha za kinyuklia.



Historia mpya imeanza sasa katika mwanzo wa amani, ulisema ujumbe ulioandikwa na Kim katika kitabu cha wageni ndani ya jumba hilo la amani huku uzito wa mkutano huo ukiwa ni wa kwanza kati ya viongozi hao wa Korea katika zaidi ya muongo mmoja.
Kim alikuwa akimtania mwenzake kuhusu tambi za baridi katika mkutano huo. ”Nadhani utapendelea sana tambi tulizoleta”, alisema. Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa inatumai kwamba mazungumzo hayo yatapiga hatua.



Mkutano huo unaonekana kuwa maandalizi ya mkutano kati ya Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump, mapema mwezi Juni, hatua isiokuwa ya kawaida kwani hakuna rais wa Marekani ambaye aliwahi kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Lengo la mazungumzo.
Lengo kuu la mazungumzo hayo ni kuzungunmzia mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini ambapo Seoul imeonya kwamba kuishawishi Pyongyang kuacha mpango wake wa nyuklia itakuwa vigumu .



Teknolojia ya Korea Kaskazini kuhusu silaha za nyuklia imepiga hatua tangu viongozi wa mataifa hayo mawili kukutana muongo mmoja uliopita. Mkutano huo, ukiwa ni wa tatu kufuatia mikutano mingine iliofanyika 2000 na 2007 unatokana na kuzidi kuimarika kwa uhusiano kati ya mataifa hayo ya Korea.


Kim alitangaza wiki iliopita kwamba atasitisha majaribio ya silaha zote za kinyuklia na hatua hiyo kuungwa mkono na Marekani na Korea Kusini, licha ya watafiti kuesema kuwa maeneo ya kujaribu silaha hizo za nyuklia huenda hayawezi kutumika tena baada ya mwamba kuanguka kufuatia jaribio la mwisho la silaha hizo mwezi Septemba.
Mbali na hilo viongozi hao wawili pia wanatarajiwa kuzungumzia kuhusu mpango wa amani ili kumaliza vita vya 1950-53 mbali na msururu wa maswala ya kiuchumi na kijamii



Ni nini kitakachofanyika?
Baada ya mkutano, wawili hao wataondoka na kupata chakula cha mchana kandokando huku ujumbe kutoka Kaskazini ukielekea katika upande mwengine wa mpaka na baadaye mchana, Bw. Moon na Kim watapanda mti kwa kutumia udongo na maji kutoka nchi zote mbili ili kuashiria amani.


Watatembea pamoja kabla ya kuanza mazungumzo mengine ambapo mkutano huo utafikia kikomo wakati viongozi hao wawili watakapotia saini makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya chakula cha jioni.



Kim Jong Un ataandaliwa viazi vya kutoka Uswizi ili kumkumbusha wakati wake alipokuwa akisomea nchini Korea Kusini pamoja na chakula cha Korea Kaskazini cha tambi baridi na mvinyo wa Korea Kaskazini.




Baada ya chakula cha jioni, ujumbe huo utatazama kanda ya video kwa jina Spring of One kabla ya Kim kurudi nyumbani.
Ni nani atakayehudhuria
Kim anaandamana na maafisa tisa, ikiwemo dadake Kim Yo-jong ambaye aliongoza ujumbe wa Korea Kaskazini katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini mapema mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog