Chadema Wakanusha Lissu Kuerejea Nchini
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mapema Januari mwaka huu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene
amesema; Kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za kwamba
Lissu anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia juzi na kwamba
amemaliza matibabu yake kitu ambacho si cha kweli na kimezua taharuki.
Makene amesema, Lissu hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote
kuhusu kurejea kwake hapa chini kwa sababu hajapona na anatarajiwa
kufanyiwa upasuaji mwingine mwishoni wiki hii au wiki ijayo.
Chadema kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote wenye
mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata Lissu
wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya matibabu na
hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo.
Lissu yupo nchini Ubelgiji akipatiwa awamu ya tatu ya matibabu
baada ya kumaliza matibabu nchini Kenya mwezi Januari ambapo alikuwepo
huko kwa takribani miezi minne ambapo alikuwa akiuguza majeraha ya
risasi zaidi ya 30 alizopigwa nyumbani kwake Dodoma, Septemba 7, mwaka
jana.
Comments
Post a Comment