RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu Yoshida wakikata utepe
kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya
Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha
lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri
wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na
viongozi wengine wa Serikali na wageni kutoka nje ya nchi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika sherehe hizo za ufunguzi wa barabara ya Iringa-Dodoma
katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika
kiwango cha lami.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi wa Iringa mjini waliofika kumpokea mara baada ya
kuwasili akitokea Isimani mkoani Iringa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefungua barabara ya lami ya Iringa – Migoli – Fufu yenye urefu wa kilometa 189 na ambayo imeunganisha mikoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma.
Comments
Post a Comment