MAMA KIKWETE, UMMY MWALIMU WATINGA HARUSI YA KIBA


MKE wa Rais wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepata fursa ya kuhudhuria katika harusi ya staa wa Bongo Fleva, Alikiba na mkewe, Amina katika ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam usiku huu wa Aprili 29, 2018.

Mama Salma ambaye pia ni mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto, Wanawake, Jinsia na Wazee, Dkt. Ummy Mwalimu katika seherehe hiyo.

Katika sherehe hiyo pia inahusisha harusi ya mdogo wa Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda ambao walifunga ndoa Jumapili iliyopita.


Viongozi wengine waliopata fursa ya kuhudhuria sherehe hiyo ni Naibu Waziri wa Kazi ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (kulia), na Mwenyekiti wa UVCCM, Khery James (kushoto).

Picha na Azama TV.

Comments

Popular posts from this blog