RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA ‘TUNAKUMISI’
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua. PICHA NA IKULU RAIS Dk. John Magufuli amesema kwa kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye uongozi wake kuna mambo makubwa ya maendeleo katika nchi yetu huku akitanguliza uzalendo mkubwa Watanzania wanamkumbuka na wataendelea kukumbuka ‘kummisi’ watake wasitake. Pia ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais mstaafu Kikwete kwani ndio amesababisha awe Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano huku akitumia nafasi hiyo kuahidi kuwa atahakikisha Serikali yake itashirikana na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)ambayo ameizindua rasmi leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi mara baada ya kumaliza kuso