Basi la Kampuni ya Maqadir Lapata Ajali Tanga
Muonekano wa ajali hiyo baada ya basi hilo kuanguka katikati ya barabara.
Basi la Kampuni ya Maqadir lililokuwa linatoka jijini Tanga kwenda
Kijiji cha Mtae, Wilaya ya Lushoto mkoani humo, limeanguka asubuhi leo
Aprili 10, 2018 katikati ya barabara kuu ya Segera-Tanga katika kijiji
cha Mpakani, kata ya Kerenge wilayani Muheza mkoani Tanga.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, majeruhi wa ajali hiyo ni mmoja na bado hajatambuliwa ambapo chanzo cha ajali hiyo, pia bado hakijafahamika.
Comments
Post a Comment