
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
MBUNGE
wa Viti Maalum (CCM) kupitia vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige amehoji kufungiwa baadhi ya nyimbo za
staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, wakati kamati ya
maudhui ilikuwepo na kuziacha nyimbo hizo zikaenda hewani kwa muda
mrefu.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Akijibu swali hilo, Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe,
amejibu kuwa Diamond siyo msanii wa kwanza kufungiwa nyimbo zake kwani
hata wasanii wa Nigeria, Davido na Wizkid, wamefungiwa nyimbo zao.
Pia alimtaja mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo, Kofii
Olomide, ambaye wimbo wake wa Ekoti Te umefungiwa nchini humo.
Pamoja na kuibuka wabunge wengi wenye kutaka kutoa taarifa na kuendelea hoja hiyo, Naibu Spika, Tulia Ackson, hakuwapa nafasi.
Comments
Post a Comment