Wanawake waliotelekezwa wadai walizalishwa na viongozi mbalimbali


WANAWAKE 480 waliotelekezwa na watoto ambao jana waliitikia wito wa kwenda kusaidiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wamesema walizalishwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kisiasa.

Hilo lilibainika baada ya wanawake hao, miongoni mwa mamia waliofika ofisini hapo  ili kupatiwa msaada wa malezi na matunzo ya watoto wao waliotelekezwa na baba zao.

Katika mfululizo wa misaada ya aina hiyo, leo wanaume waliotelekezewa watoto na mama zao, watafika ofisini kwa mkuu wa mkoa huyo kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa suala hilo.

Wakati huohuo, Makonda akihutubia wakati wa uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 unaofanyika leo katika viwanja vya Zakeem Mbagala, amesema wanawake 47 waliofika ofisini kwake jana wanadai wabunge ndiyo wamewatelekeza na watoto na wengine  wamesema  wamezalishwa na kutelekezwa na viongozi wa dini mbalimbali.

Katika hafla hiyo ya utoaji wa chanjo, mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais Samia Suluhu.

Comments

Popular posts from this blog