Posts

Mtanzania Mahakamani Uingereza Akidaiwa Kumuua Mkewe

Image
Raia wa Tanzania Kema Salum. RAIA wa Tanzania Kema Salum (38) amefikishwa mahakamani nchini Uingereza akidaiwa kumuua mkewe, Mtanzania pia, aitwaye Leyla Mtumwa. Salum anayedaiwa kumchoma visu Leyla na kumuua wakiwa nyumbani kwao mtaa wa Kirkstall, Haringey, nchini humo Ijumaa iliyopita, amefikishwa katika mahakama ya Crown. Marehemu Leyla Mtumwa. Kutokana na mgomo wa wanasheria nchini humo tangu kuanza kwa mwezi Aprili, kesi hiyo haikusikilizwa na Jaji Anuja Dhir ameahirisha usikilizwaji wake hadi Juni 20 mwaka huu. Kwa mujibu wa mwanasheria Seona White, juhudi zinafanyika ili kupata wakili wa kumtetea Salum mahakamani licha ya mgomo wa mawakili unaoendelea. Mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka yake kwa Kiingereza lakini kupitia mkalimani aliyemwelewesha kwa Kiswahili. Mipango inafanywa kumleta marehemu nchini Tanzania.

JPM Awalilia 12 Waliokufa Ajalini Tabora, Ataka Polisi Kujitathmini

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12 vilivyotokea katika ajali ya basi kugongana na lori Kijiji cha Makomero, Wilaya Igunga mkoani Taborausiku wa kuamkia leo.

Hatma ya Nabii Tito aprili 13

Image
KESI  inayomkabili Tito Machibya maarufu Nabii Tito, hatma yake kujulikana Aprili 13 mwaka huu baada ya mahakama ya Wilaya ya Dodoma kupokea taarifa za kitabibu jana asubuhi. Mahakama ya Wilaya ya Dodoma jana ilipokea taarifa ya vipimo vya kitabibu vya Tito Machibya, ilivyokuwa imeviagiza hapo awali na kumtaka afanyiwe vipimo katika Taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma. Jana Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha alisema mahakamani hapo kuwa alipokea taarifa ya kitabibu kuhusu Nabii Tito kutoka Taasisi ya Isanga hivyo ataipitia na kutoa maamuzi siku hiyo ya Aprili 13. “Nieleze kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa huyu leo asubuhi hivyo nitaipitia ili April 13 mwaka huu siku ya Ijumaa niweze kuitolea maamuzi,” alisema Karayemaha. Hata hivyo Nabii Tito jana aliweza kuhudhuria mahakamani akitokea mahabusu ya gereza kuu la Isanga baada ya kutofikishwa mahakamani  hapo  mara mbili mfululizo. Aidha ba

Mbasha afunguka ishu ya kumpa mimba Agness

Image
Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa alizozipata kuwa amempa ujauzito msichana anayevuma kwenye mitandao ya kijamii Agness na kudai hana mahusiano yeyote na mtu huyo zaidi ya kumfahamu kupitia mitandaoni. Mbasha amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu zinazozidi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa zinadai kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi na mpaka kufikia hatua ya kukubalia kupeana ujauzito. "Agness mimi namfahamu kama shabiki yangu kupitia mitandao ya kijamii. Sasa sielewi mambo yamegeuka vipi mpaka kufikia hatua ya kuambiwa mimi nina mahusiano naye. Sijawahi kuwa na mahusiano na Agness na wala sijawahi kuwa na chochote kile kinachoashiria mapenzi", amesema Mbasha. Pamoja na hayo, Mbasa ameendelea kwa kusema "sitegemei kupata naye mtot

Ndugai: Bashe Apeleke Hoja Yake Kwenye Chama Kabla ya Bungeni

Image
Bashe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai amesema suala la Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe kutoa hoja binafsi bungeni, alitakiwa kuipeleka kwenye chama chake kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kuipeleka bungeni. Ndugai amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu. Amesema Kanuni za Bunge zipo na Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na zipo, kama kwa wabunge wa kambi ya upinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za Bunge. Ndugai. Amesema Bashe kama mbunge wa CCM, kanuni za wabunge wa CCM zinamtaka aipeleke hoja yake kwenye chama chake kwanza, ikajadiliwe huko na ikikubaliwa Bunge liweze kuipokea. Amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo kutoka kwa Bashe, pia halijapokea taarifa kutoka kwa katibu wa wabunge wa CCM kama wameipokea hoja hiyo na wameshaurianaje. Mwezi uliopita, Bashe alisema amemuandikia barua

Watu wanne wadakwa kwa tuhuma za wizi katika Ujenzi wa reli ya kisasa

Image
Watu wanne wanashikiliwa na Polisi Ngerengere, Mkoani Morogoro wakituhumiwa kuhusika na wizi wa lita 2510 za mafuta aina ya Dizeli kutoka kambi ya ujenzi wa reli ya kisasa Standard Geuge. Watuhumiwa hao wamekamatwa na polisi kikosi maalumu cha reli nchini kwa kushirikiana na maafisa wa shirika la reli Tanzania ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika. Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Kikosi Maalumu cha Reli Salum Kisai, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao itakuwa fundisho kwa watanzania wengine wanaofanya kazi katika mradi huo ili kuweza kulinda mali za mkandarasi na kumaliza kwa mradi huo kwa muda unaotakiwa. Kwa upande wake Afisa wa shirika la Reli nchini TRC Catherine Mushi, amesema wananchi wanapaswa kushiriki katika kulinda miundo mbinu ya reli hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza uaminifu kwa wawekezaji nchini kuweza kutoa ajira zaidi kwa watanzania.

Breaking News: Winnie Mandela afariki dunia

Image
Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake. Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe - Nelson Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw Mandela. Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27. Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata. Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa. Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa. Kujitolea kwakena ukakamavu wake vilionekana mumewe alipofungwa jela maisha mwaka 1964 na akaachwa kuendeleza harakati za kisiasa. "Kamwe sitakata tamaa na watu wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila shaka tunatarajia kwamba kazi

WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI GEITA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo, Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018

Sababu Za Kuwashwa Baada Ya Kuoga

Image
      “Wataalamu wa afya ya ngozi pia wanabainisha kuwa kuoga muda mrefu na mara kwa mara, matumizi ya sabuni zenye harufu kali na povu jingi ni mambo mengine yanayochangia kutokea kwa mzio pamoja na ukavu wa ngozi kutokana na uwezo wake wa kuondosha kiasi kikubwa cha mafuta yanayolinda ngozi. Ili kupunguza hali ya muwasho, “Tumia sabuni zenye mafuta, lakini zisiwe na marashi makali.” Katika hali ya kawaida kitendo cha kuoga kinapaswa kuchukuliwa kama jambo la kufurahisha kutokana na ukweli kwamba huufanya mwili uburudike na kuwa safi. Lakini kwa baadhi ya watu mambo ni tofauti. Kuoga huwa sawa na karaha. Moja ya matatizo ya kiafya ambayo yanayosumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha mara baada ya kuoga. Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu. Hali hii inaweza kuwa inajitokeza kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu, hili linaweza kuwa t

Sakata la Wambura lafikia Patamu

Image
RUFAA ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura, sasa imefikia patamu baada ya juzi Jumamosi kusikilizwa katika makao makuu ya shirikisho hilo, Karume jijini Dar es Salaam na hivi sasa watu wengi wanataka kujua nini kinachofuatia. Hivi karibuni, Wambura alikata rufaa Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kupinga maamuzi ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo ya kumfungia maisha kujihusisha na soka kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine. Wakili wa Wambura, Emmanuel Muga, ameliambia C hampioni Jumatatu kuwa, kamati hiyo iliziita pande mbili zote zinazochuana katika sakata hilo na kuzisikiliza kwa umakini mkubwa. Alisema katika kikao hicho, mambo yalienda vizuri, kwa hiyo kinachosubiriwa tu hivi sasa ni maamuzi ya hiyo kamati. “Kamati imesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura, vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na mustakabali mzima wa kesi hiyo. Kwa hiyo tun

Mamba akutwa katika bwawa la kuogelea Florida, Marekani

Image
Polisi katika jimbo la Florida, Marekani wamesema mamba wa urefu wa futi 11 alipatikana kwenye bwawa la kuogelea la familia moja katika jumba hilo. Polisi wamepakia picha za mamba huyo mtandaoni, Wakazi wa Nokomis waliwapigia simu polisi na kuomba usaidizi baada ya kumgundua mnyama huyo. Afisa wa polisi wa eneo la Sarasota alipakia mtandaoni picha ya afisa wa wanyama aliyeitwa kumnasa akiwa anamburuta mnyama huyo kutoka kwenye maji Jumamosi. Polisi wanasema mamba huyo alifanikiwa kupita kwenye uzio uliokuwepo na kuingia kwenye bwawa hilo, Mamba nchini Marekani kwa kawaida hukua hadi kuwa na futi kati ya 11 na 15 na wanaweza kuwa na uzani wa kilo 454. Mamba wa Marekani hupatikana mashariki mwa Marekani katika majimbo ya Florida na Louisiana, kila jimbo likiwa na zaidi ya mamba milioni moja. Eneo la kusini mwa Florida ndilo pekee ambalo mamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi kwa pamoja. Ingawa awali walikuwa wameorodheshwa kama wanyama walio hatari

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo

Image
Bonyeza links zifuatazo Kusoma zaidi na Kuapply: 200+ Vacancies in Public and Private institutions in Tanzania, March 2018 Job Opportunity at the US Embassy Tanzania: Chauffeur Job Vacancy at Save the Children Tanzania - FINANCE ASSISTANCE Job Opportunity at UN Organization - Consultancy Process Expert Volunteer Job Opportunity at UN Organization - Marketing & Promotional Materials Expert Volunteer Job Opportunity at UNHCR - Registration Officer Job Opportunity at a Reputable NGO - Consultant to Conduct Assessment of BEST-Dialogue Support to Print Media Job Opportunity at Plan International Tanzania Nafasi zingine ingia  www.ajirayako.co.tz

Gabo, Wema na Kitale walivyoshinda tuzo za SZIFF April 1

Image
Usiku wa April 1 2018 Mlimani City Dar es Salaam zilifanyika tuzo za Sinema Zetu International Film Festival SZIFF na kuhudhuriwa na mastaa na watu mbalimbali kutoka tasnia tofauti tofauti. Rais mstaafu wa awamu ya nne Dr Jakaya Mrisho Kikwete ndio alikuwa mgeni rasmi na alishuhudia tuzo 19 zikitolewa kwa wasanii wa filamu, watayarishaji, wahariri na wabunifu wa sound track za movie hiyo. Miongoni mwa mastaa wa filamu waliyofanikiwa kushinda tuzo hizo ni pamoja na muigizaji Wema Sepetu aliyeshinda tuzo mbili za Best Actress na People’s Choice Award na Gabo ambaye ameshinda tuzo ya Best Actor huku Kitale akishinda tuzo ya Best Comedian. Alichozungumza Wema Sepetu baada ya ushindi wa tuzo ya Best Actres s

Aamka na kukuta Jeneza Nje ya Nyumba!

Image
MBEYA:  NELSON Edson, mkazi wa Mtaa wa Nsalaga Kata ya Nsalaga jijini hapa amejikuta kwenye taharuki kubwa baada ya kuamka na kukuta jeneza tupu dogo nje ya mlango wa nyumba yake. Tukio hilo lililoibua hekaheka mtaani hapo lilijiri asubuhi ya Machi 27, mwaka huu. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Nsalaga, Paul Ngonde, alipokea taarifa kutoka kwa Edson na kuamua kwenda eneo la tukio ili kushuhudia. Alisema kuwa, baada ya kuwashirikisha wazee wa mila juu ya jambo hilo, walilifungua jeneza hilo na kukuta likiwa tupu, lakini likiwa na sanda nyeupe iliyoviringishwa ndani yake. “Nimeshangaa asubuhi kuamka na kukuta jeneza nje ya mlango wa nyumba yangu, sijaelewa ni nini madhumuni ya kuwekewa jeneza hilo,” alisema Edson huku akionesha kustaajabishwa na tukio hilo. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mtaa huo umekuwa na matukio ya ajabuajabu yakiwemo ya kutupa watoto, lakini tukio hilo la jeneza limekuwa ni tukio la kwanza kutokea mtaani kwake.   Kwa upande wake, Kamanda wa P

“Kuna kitu MUNGU anataka kutuambia kupitia Waraka wa Maaskofu” Askofu Shoo

Image
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli, Askofu  Frederck Shoo amewata baadhi ya watu kuacha  kupotosha ukweli wa waraka wa maaskofu kwa kuupaka matope na kusema anae fanya hivyo  ni mjinga. Askofu Shoo ametoa kauli hiyo leo April 1, 2018 katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini, mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Pasaka. Askofu Shoo amenukuliwa akisema   “Wapo wanaotumia nguvu nyingi kutaka kupotosha ujumbe wa waraka wa Maaskofu na wamekuwa wakilipaka Kanisa matope ili waweze kurejea katika waraka ule, watu hawa naweza kuwaita ni wajinga lakini pamoja na hilo nataka wakayatafakari na kama wanaona kuna hatua za kuchukua wachukue.”   “Kanisa limekuwa linapata kejeli za aina mbalimbali kutoka kwa watu hao na kuwatuhumu kuwa maskofu walifikia maamuzi ya kuandika waraka huo kutokana na sababu za kimaslahi kwa maana ya sadaka makanisani kupungua jambo ambalo si la kweli.” -As

Mpenzi wa Cristiano Ronaldo ametumia Kiswahili leo

Image
Lugha ya Kiswahili inaonekana kuzidi kukuwa na kuwavutia watu mbalimbali dunia kuitumia, leo April 1 2018 moja kati ya post za mitandao ya kijamii zilizochukua headlines ni post ya mwanamitindo  Georgina Rodríguez ambaye ni mpenzi wa staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Georgina Rodríguez ni mwanamitindo na ndio mpenzi wa sasa wa Ronaldo na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Alana Martina , hivyo katika insta story yake amepost picha yake na Ronaldo na kuandika ‘Hakuna Matata’ Msemo wa hakuna matata ni msemo wa Kiswahil i ambao umeonekana kupendwa na umekuwa msemo maarufu sana kwa wageni wanaopenda kujua lugha ya Kiswahili, huo huwa ni msemo wao wa kwanza kujifunza lakini haijajulkana bado  Georgina Rodríguez ameujulia wapi msemo huo.

PRETTY KIND AWAIBUA WABONGO TENA,KISA MABADILIKOYA AJABU

Image
Mrembo Suzan Michael ‘Pretty Kind’ aliyekuwa Bingwa wa picha za utupu mtandaoni ameonesha kubadilika kitabia hasa katika mitandao ya kijamii na hilo limeonekana baada ya kuanza kuutumia mtandao wake wa kiijamii wa Instagram. _ Ikiwa ni siku chache za msanii huyo kuwa huru baada ya kusamehewa kwa adhabu yake ya kifungo cha kutojihusisha na masuala ya muziki kwa muda wa miezi sita kutokana na hatua za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo dhidi ya kukiuka maadili kupitia Naibu wa wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza mwezi Januari mwaka huu.   Hizi ni picha baadhi za Msanii huyo ambazo anaonekana kubeba kitabu kitakatifu ‘Biblia’ na kuandika kuwa Mwenyezi Mungu kwa sasa anaweka sawa mambo ya kila kilichotoka katika mstari wake.

Rais Magufuli Aungana na Wakristo Kuadhimisha Misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Dar

Image
Rais Magufuli leo ameungana na Wakristo wote Tanzania katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakilakiwa kwa furaha na Paroko Msaidizi Venance Tegete walipojumuika na waumini wengine katika Maadhimisho ya Misa ya Sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na waumini wengine wakisikiliza kwa makini mahubiri ya Paroko Msaidizi Venance Tegete katika Maadhimisho ya Misa ya Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka katika Maadhimis

Meli ya abiria ya Uingereza iliyozamishwa mwaka 1942 yaondolewa baharini

Image
Meli ya abiria ya Uingereza iliyozamishwa wakati ilishambuliwa kwa bomu na ndege za Japan wakati wa vita vya pili vya dunia, imeinuliwa kutoka baharini pwani mwa Sri Lanka baada ya miaka 75. SS Sagain, ambayo abiria wake wengi na mizigo iliokolewa mwaka 1942, imeinuliwa na kundi la wapiga mbizi kutoka kwa jeshi la wanaji wa Sri Lanka, Ilikuwa karibu umbali wa futi 35 chini ya bahari katika bandari ya Trincomalee. Shughuli ya kuiinua meli hiyo ilichukua miezi kadhaa na ilifanywa na kikosi cha wanamaji cha Mashariki mwa Sri Lanka.

RAY C ATIBUKA VIBAYA,ATOA MANENO TATA KISA LADY JAY DEE,ASEMA BORA ATIWE MIMBA AZAE

Image
Muimbaji Ray C amefunguka mazito kwa kile anachoona kinaenda ndivyo sivyo katika muziki wa Bongo Flava kwa sasa. Ray C amefikia hata hatua ya kutumia maneno makali kueleza hisia zake kwa yale ambavyo hakubaliani nayo kwenye tasnia hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; Kuna muda huwa nafikiria mambo mengi sana! kuna muda najiskia kuamua kutiwa mimba, nizae niwe tu mama wa nyumbani! maana kuna muda nikiangalia wasanii wenye maendeleo kwenye Bongo Flava ni wachache saaaaana! na sijiongelei mimi maana mimi mwenyewe kuna wakati nilivurunda mwenyewe! Nakubali nilibugi na nikagundua nimebugi haswa na ndio maana nimepambana mpaka hapa niliko baada ya kugundua baraka tele nilizozawadiwa na Mungu ni kubwa mno kuliko starehe za muda za ndogo na za kibwege!!! Ila huwa nakaa najiuliza miaka kama sita ambayo nilipotea kwenye industry! kuna wasanii nilianza nao na wana vipaji vya ajabu maskini lakini wengi wao wamezimwa kama taa!!! Namkumbuka Nature, Joseline, B