Mtanzania Mahakamani Uingereza Akidaiwa Kumuua Mkewe
Raia wa Tanzania Kema Salum.
RAIA wa Tanzania Kema Salum (38) amefikishwa mahakamani nchini Uingereza akidaiwa kumuua mkewe, Mtanzania pia, aitwaye Leyla Mtumwa.
Salum anayedaiwa kumchoma visu Leyla na kumuua wakiwa nyumbani kwao mtaa wa Kirkstall, Haringey, nchini humo Ijumaa iliyopita, amefikishwa katika mahakama ya Crown.
Marehemu Leyla Mtumwa.
Kwa mujibu wa mwanasheria Seona White, juhudi zinafanyika ili kupata wakili wa kumtetea Salum mahakamani licha ya mgomo wa mawakili unaoendelea.
Mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka yake kwa Kiingereza lakini kupitia mkalimani aliyemwelewesha kwa Kiswahili. Mipango inafanywa kumleta marehemu nchini Tanzania.
Comments
Post a Comment