Ndugai: Bashe Apeleke Hoja Yake Kwenye Chama Kabla ya Bungeni
Bashe.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai
amesema suala la Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe kutoa hoja
binafsi bungeni, alitakiwa kuipeleka kwenye chama chake kwa ajili ya
kujadiliwa kabla ya kuipeleka bungeni.Ndugai amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu. Amesema Kanuni za Bunge zipo na Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na zipo, kama kwa wabunge wa kambi ya upinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za Bunge.
Ndugai.
Amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo kutoka kwa Bashe, pia halijapokea taarifa kutoka kwa katibu wa wabunge wa CCM kama wameipokea hoja hiyo na wameshaurianaje.
Mwezi uliopita, Bashe alisema amemuandikia barua Katibu wa Bunge kuhusu ombi la kuwasilisha hoja binafsi bungeni ya kutaka kuundwa tume teule itakayochunguza matukio ya kihalifu yanayofanyika nchini.
Kuhusu afya yake, Ndugai ameeleza kwamba imeimarika kulinganisha miezi michache nyuma.
CREDIT: AZAM TV
Comments
Post a Comment