PRETTY KIND AWAIBUA WABONGO TENA,KISA MABADILIKOYA AJABU

Mrembo Suzan Michael ‘Pretty Kind’ aliyekuwa Bingwa wa picha za utupu mtandaoni ameonesha kubadilika kitabia hasa katika mitandao ya kijamii na hilo limeonekana baada ya kuanza kuutumia mtandao wake wa kiijamii wa Instagram. _
Ikiwa ni siku chache za msanii huyo kuwa huru baada ya kusamehewa kwa adhabu yake ya kifungo cha kutojihusisha na masuala ya muziki kwa muda wa miezi sita kutokana na hatua za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo dhidi ya kukiuka maadili kupitia Naibu wa wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza mwezi Januari mwaka huu.
 
Hizi ni picha baadhi za Msanii huyo ambazo anaonekana kubeba kitabu kitakatifu ‘Biblia’ na kuandika kuwa Mwenyezi Mungu kwa sasa anaweka sawa mambo ya kila kilichotoka katika mstari wake.

Comments

Popular posts from this blog