Posts

Image
 Msanii wa muziki Bongo,Ambwene Yesaya maarufu kama AY amefunga ndoa leo na mpenzi wake wa muda mrefu Remy. Shughuli za kufunga ndoa hiyo zimefanyika leo katika hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar Es Salaam na kuhudhuliwa na mastaa mablimbali kama vile:-Lady Jaydee, Mwana FA, Salama Jabir, Profesa Jay (Joseph Haule), Fid Q na wengineo wengi.

BREAKING : MFANYAKAZI AKUTWA AMEGANDA KWENYE FREEZER MWAKA 1 TANGU APOTEE

Image
Jeshi la Polisi nchini Lebanon limemkamata mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Nader Essam Assaf ambaye amekutwa na mwili wa mfanyakazi wake wa ndani akiwa amekufa ambaye alikuwa ni raia wa Ufilipino. Mwili wa marehemu huyo Joanna Demafelis, 29, umekutwa ukiwa umewekwa kwenye jokofu (freezer) ndani ya nyumba ya mwajiri wake huyo, mwaka mmoja baada ya kuripotiwa kuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo cha binti huyo kimesababisha vurugu nchini Ufilipino ambapo kumesababisha kufungwa kwa safari ya kwenda kufanya kazi Kuwait, Lebanon. Mtuhumiwa huyo Assaf na mkewe Mona wanatuhumiwa kuhusika na kifo hicho cha binti huyo. Hatahivyo mwanamke huyo bado hajapatikana kutokana na kwamba yuko mafichoni kufuatia tukio hilo.

Kauli ya Zitto Kabwe baada ya kuachiwa

Image
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuwataka watu wasirudishwe nyuma kwa vitisho na usumbufu wa sheria kandamizi zinazopelekea baadhi ya viongozi kukamatwa na kuwekwa ndani. Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23, 2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo. "Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo" alisema Zitto Kabwe Aidha Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambap...

Vigogo waliokamatwa kwa amri ya RC Mnyeti wahamishiwa Babati

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga   Vigogo watano wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro na jijini Arusha, walioshikiliwa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, wakidaiwa kudhamini uchimbaji haramu wa madini hayo, wamepelekwa mjini Babati chini ya ulinzi wa polisi. Wiki mbili zilizopita Mnyeti aliagiza vigogo hao wa madini kukamatwa na kushikiliwa kwa saa 48 kwenye kituo cha polisi Mirerani wakidaiwa kufadhili uchimbaji huo haramu. Akizungumza leo Februari 23, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amethibitisha vigogo hao wa madini kusafirishwa licha ya kuwa walipatiwa dhamana, polisi wakawashikilia na kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo. Amesema waliwashikilia wachimbaji hao baada ya kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa huo kupata taarifa kuwa vigogo hao wanashiriki kuwadhamini vijana wanaoingia kwa wizi kwenye migodi ya kampuni ya TanzaniteOne yenye ub...

BREAKING : POLISI AUAWA KWENYE VURUGU ZAMASHABIKI

Image
Afisa Polisi mmoja amefariki hapo jana kufuatia vurugu zilizofanywa na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Spartak Moscow dhid ya wale wa timu ya Athletic Bilbao kabla ya mchezo wa Europa League hapo jana siku ya Alhamisi. Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuwasha baruti zilizokuwa zikiwaka katika mitaa zilizosababisha baadhi ya mashabiki wa Bilbao kufikishwa hospitali. Kufuatia machafuko hayo askari polisi mmoja alifariki kutokana na shinikizo la moyo. Msemaji wa jeshi la polisi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho huku akishindwa kueleza chanzo cha umauti wake. Askari huyo alifariki baada ya kufikishwa hospitalini kwaajili ya matibabu8 kufuatia kupata shinikizo la moyo wakati akijaribu kutuliza vurugu za mashabiki eneo la Basque. Shirikisho la soka barani Ulay (UEFA) limesema kuwa limesikitishwa na tukio hilo lililojitokeza huko Bilbao usiku wa siku ya Alhamisi.

Zitto Aachiwa kwa Dhamana, Atoa Kauli Mauaji ya Diwani

Image
KIONGOZI Mkuu wa  ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno ya Sh. 50 milioni na kudhaminiwa na wakili wake, Lazarus Mvula baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi Morogoro tangu jana Alhamisi kwa kufanya mkusanyiko bila kibali. Zitto alikamatwa katika Kata ya Kikeo wilayani Mvomero na alitarajiwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dakawa lakini akahamishiwa Morogoro Mjini. “Muda huu ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh50milioni. Anatakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018,” inaeleza taarifa ya wakili wake. Aidha, Zitto amefungukia mauaji ya Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Mwandishi wa Gazeti la Uhuru ajeruhiwa Ajali ya Malori

Image
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, amejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam, usiku huu baada ya gari dogo alilokuwa akiliendesha lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT. Kwa mujibu wa dereva wa lori la mafuta lililohusika katika ajali, William Colonel, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupanda kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta na gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda. Lori la mafuta na gari dogo yote yalikuwa upande wa kushoto wa barabara. Imeelezwa lori hilo baada ya kuanguka lililibana gari dogo lililokuwa katikati. Shuhuda wa ajali hiyo, Adeodatus Sylivester Charles amesema "Nilimtambua majeru...

JPM: Mtanisamehe, Mimi Siyo Mwanasiasa Mzuri!

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa yeye si mwanasiasa mzuri ndiyo maana lugha yake siku zote si nzuri. Magufuli amesema hayo leo Februari 22, 2018 wakati akihotubia katika mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao unaendelea sasa Kampala nchini Uganda ambapo Marais wa nchi hizo wamekutana huko kujadili mambo mbalimbali ambapo Rais Magufuli amewataka viongozi hao kuangalia changamoto mbalimbali ambazo zinazikabili nchi hizo. “Mtanisamehe lugha yangu siyo nzuri kwa kuwa mimi siyo mwanasiasa mzuri, tunataka kutengeneza viwanda yaani kuzifanya nchi zetu ziwe za viwanda tutaweza kushindana na nchi ambazo gharama yake ni 0.12 wakati sisi ni zaidi ya mara kumi ya hiyo hayo ni maswali ambayo sisi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kila mmoja wetu lazima tujiulize je tutafika hapo hizo ndiyo changamoto lakini pia gharama za umeme zinasababisha gharama za uzalishaji kuongezeka na kupelekea pato l...

Rais wa FIFA atoa ahadi hii kwa Majaliwa

Image
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino amemwahidi Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kuwa FIFA itawekeza katika miradi ya maendeleo ya soka nchini. Infantino ametoa ahadi hiyo jana katika mazungumzo yake maalum na Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa ofisini kwake baada ya kumtembelea ikiwa ni sehemu ya ratiba zake nchini baada ya kumaliza mkutano mkuu wa FIFA wa mwaka wa kikanda. Kwa upande wake Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania inaunga mkono juhudi za FIFA katika kupambana na rushwa kwenye soka pamoja na matumizi mabaya ya fedha na madaraka. Rais huyo aliyechukua mikoba ya Mswisi Joseph ‘Sepp’ Blatter Februari 26 mwaka 2016 ameunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kupambana na rushwa katika sekta ya michezo. Aidha Infantino ameishukuru Serikali kwa ukarimu wake na kumuomba Waziri Mkuu Majaaliwa kufikisha salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Po...

Breaking News: Diwani Chadema Auawa Usiku Morogoro

Image
Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana. Kwa mujibu wa mbunge wa Kilobero, Peter Lijualikali amesema; Taarifa za awali zinasema kuwa usiku huu umeme ulikatika katika nyumba yake. Luena akatoka nje kutizama kama kuna shot maana nyumba za jirani zilikuwa na umeme. Alipozunguka nyuma ya nyumba yake kukagua umeme akalutana na kikosi cha watu wenye mapanga wakamkatakata hadi wakamtoa roho. Ameandika Mbunge wa Mikumi @professorjaytz ameandika; “Diwani wetu wa Chadema Kata ya Namwawala, Jimbo la MLIMBA (MOROGORO) GODFREY LUENA ameuawa usiku huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana,   R.I.P. LUENA.” Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limethibitisha kutokea kwa kifo hicho; “Ni kweli diwani Luena ameuawa usiku wa huu, polisi wameshafika eneo la tukio wanaendelea na uchunguzi lakini ni mapema sana kutoa majibu k...

MGUU WA MTOTO WANASA KWENYE NGAZI ZA UMEME AIRPORT

Image
Mtoto Julian ambaye mguu wake ulinaswa kwenye ngazi za umeme kwenye uwanja wa ndege wa Vancouver, Canada. Mama yake, Andrea Diaczok, ametoa wito kwa wazazi kuwa macho na watoto wao katika sehemu hizo. MTOTO Julian mwenye umri wa miaka miwili alijikuta akivunjwa mifupa ya mguu wake uliponasa kwenye ngazi za umeme katika kiwanja cha ndege cha Vancouver, Canada. Kiatu cha Julian kikiwa katika mashine za ngazi za umeme kilipokuwa kimenasa. Julian alikuwa na wazazi wake, Andrea Diaczok, mama yake,  na baba yake, Jeff Lee walikuwa wakirejea mjini Calgary wiki iliyopita kutokea Vancouver.  Mguu wa mtoto huyo ulikwama pembeni kati ya ngazi na vyuma vinavyozungusha mikanda inayopandisha abiria. Julian akiwa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu, kinyume na woga wa wazazi wake ambao walifikiri huenda mguu wake ungekatwa. “Mguu wake ulipotea kabisa kwenye mkanda unaozunguka,” Diaczok, alisema na kuongeza kwamba kuona hivyo alipiga kelele kwa nguvu. Waz...

Mtanzania Akamatwa na Dhahabu ya Bilioni 2, Nairobi

Image
MWANAMME mmoja anayedaiwa kuwa ni raia wa Tanzania amekamatwa na maofisa wa forodha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya, akisafirisha dhahabu ya thamani ya dola milioni moja (sawa na zaidi Tsh. Bilioni 2) taarifa zinasema. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 46 anadaiwa kuingia Nairobi akitokea mkoani Mwanza, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) na alikuwa safarini kuelekea Dubai. Gazeti la Nation limesema mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halijajulikana hadi  sasa, aliwasili uwanja wa JKIA, Ijumaa, Februari 16 na  ndege ya Precisio Airlines akitaka kuunganisha na ndege ya Kenya Airways kuelekea Dubai kabla ya kukamatwa na kuhojiwa na Maofisa wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai nchini humo na wachunguzi kutoka Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA). Sheria za Usimamizi wa Forodha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za mwaka 2004, Kifungu 85(3) na Kiambatisho cha Pili Sehemu B (4) huharamisha usafirishaji wa madini ...

Breaking: Ripoti ya TRA Kuhusu Utajiri wa Kakobe, Amuomba Radhi JPM

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema wakati wakiendelea kumchunguza Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel, Zachary Kakobe , mnamo Januari 24, 2018, Askofu huyo alimuandikia barua Rais Dkt. John Magufuli kumuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi na matamshi ya dharau kuwa ‘ana pesa nyingi kuliko Serikali’. Hayo yamesemwa leo na Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere , wakati akizunumza na wanahabari jijini dar es Salaam akitoa ripoti ya uchunguzi huo. Akihubiri wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi, Desemba 24, mwaka jana, askofu huyo alisema yeye ni tajiri zaidi ya serikali ya Tanzania na baadaye kusema kuwa utajiri anaomiliki kwa sasa ni zaidi ya serikali nyingi duniani jambo ambalo liliwafanya TRA wamchunguze.

RATIBA KUAGWA MWILI WAMAREHEMU AKWILINA DAR

Image
BAADA ya maridhiano ya kuuchukua mwili katika Hospitali ya Taifa Mhimbili, familia ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi imetoa ratiba ya kuagwa kwa mwili w binti huyo. Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya mwili wa marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kaka wa marehemu, Moi Kiyeyeu alisema kuwa mdogo wake ataagwa Alhamisi hii Februari 22, katika viwanja vya Chuo cha NIT kilichopo Mabibo jijini Dar na baadaye atasafirishwa kwenda nyumbani kwao Rombo-Mashati mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, ripoti ya uchunguzi waliyopewa na madaktari wa Muhimbili inaonesha kuwa marehemu alipigwa risasi kichwani iliyoingia upande wa kushoto na kutokea upande wa kulia. “Ripoti tuliyopewa inaonesha kichwa cha marehemu kilipasuliwa na risasi ambayo iliingia upande wa kushoto na kutokea upande wa kulia ambao umefumuliwa vibaya,” shemeji wa Akwilina, Festo Kavis...

Mbowe, Mashinji, Mnyika na Wengine 4 Waitwa kwa DCI Kuhojiwa

Image
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na viongozi wengine 6 wa chama hicho wameitwa rasmi Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa. Viongozi hao wanatuhumiwa kwa kufanya maandamano kinyume cha sheria kwa mujibu wa barua hiyo ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi. Viongozi wengine 6 walioitwa ni; – Dkt Mashinji(Katibu Mkuu wa CHADEMA) John J. Mnyika(Mbunge na Naibu Katibu Mkuu Bara) Salum Mwalim(Naibu Katibu Mkuu ZNZ) Halima Mdee(Mbunge na M/Kiti wa BAWACHA) John Heche(Mbunge) Ester N. Matiko(Mhazini wa BAWACHA).

ZARI KUMPIGA KIBUTI DIAMOND KWAIBUA MAMBO MAPYA,KWANINI ZARI KAUMIZWA UJEREO WA WEMA SEPETU NA SI HAMISA MOBETO

Image
SIKU chache baada ya Zarinah Hassan ‘Zari Boss Lady’ kuweka wazi kuwa ameachana na baba watoto wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, swali linakuja ni kwa nini Zari anaweza kuwa ameumizwa sana na Wema Abraham Sepetu na si Hamisa Mobeto ambaye hivi karibuni amempa msongo wa mawazo baada ya kuzaa na baba watoto wake? Twende taratibu! Kwanza nauliza swali hilo ambalo nitaliweka wazi baadaye kidogo na kadiri unavyoendelea kusoma makala haya, utanielewa. Baada ya matukio yote ya Diamond na Mobeto, bado Zari alionekana kuwa ‘jiwe’ na kutetea penzi lake lakini lilipokuja suala la shoo ya Mboso ambayo Diamond alionekana wazi kuwa na mahaba na Wema kwa video yao ya ‘kupapasana’ kuwekwa mitandaoni, siku chache baadaye Zari aliamua kutangaza rasmi kummwaga Diamond. Sababu ya wadau na mashabiki wa Baba Tiffah na Mama Tiffah kuona kuwa hiyo itakuwa imemuudhi Zari ni jinsi wapendanao hao walivyopotezeana hata kabla ya Zari kutangaza kuachia ngazi na muda mwingi akaonekana kuu...

Mke na Mme Waliokamatwa na Madawa China, Familia Yaanika A-Z

Image
Baraka Malali na mkewe pamoja na mtoto wao. Sakata la Watanzania wawili ambao ni mke na mume kukamatwa na dawa za kulevya ‘unga’ nchini China na mtoto wao kurudishwa Bongo , limeingia sura mpya, baada ya familia za pande zote mbili kuzungumza na siri ya safari yao kufichuka, Ijumaa Wikienda lina ukweli wa tukio hilo. Wakazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam , Baraka Malali na mkewe Ashura Musa walikamatwa Januari 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Baiyun jijini Guangzhou, China wakiwa wamemeza jumla ya pipi 129 za dawa za kulevya zilizosadikika kuwa ni heroin. Mume alipakia pipi 47 na mkewe pipi 82. Taarifa zilieleza kuwa, mamlaka nchini humo ziliamua kumrudisha nyumbani mtoto wao ambaye aliwasili Bongo wikiendi iliyopita kukabidhiwa kwa Ustawi wa Jamii, wakati mipango ya kumkabidhi mtoto huyo kwa ndugu wa wazazi wake ikiendelea. Baada ya kujiri kwa tukio hilo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na wazazi wa watuhumiwa hao na Idara ya Ustawi wa Jamii kujua kw...

Breaking News: Salum Mwalimu Akamatwa na Polisi

Image
Mgombea ubunge wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu. MGOMBEA  ubunge wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu amekamatwa na polisi kituo cha kupigia kura cha Idrisa Kata ya Magomeni. Akizungumza na Global TV Online mchana huu Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kukamatwa kwa mgombea huyo.

Diamond Platnumz ateswa na maamuzi ya Zari

Image
 Leo February 16,2018 Diamond Platnumz ameonekana kuonyesha hisia zake juu ya maamuzi  ya Zari kuachana nae, kupitia instagram account yake Diamond amekuwa akipost video clips mbalimbali za nyimbo za mapenzi. Kupitia instagram ya Diamond Platnumz amepost kipande cha wimbo wake wa Sikomi na kuandika “Unajua Nyimbo zingine Unaziimba ila Hata we mwenyewe zinakuingia Baadae😟…. Anyways 28 Days Before the Reveal of #AboyFromTandaleAlbum!🔥 #SikoMi Bonus Track on #AboyFromTandale Available on All Digital Platforms now!”

Wananchi Wamkataa Mkuu Wa Wilaya Mbele Ya Waziri Mkuu

Image
WANANCHI wa wilaya ya Kwimba wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na mkuu wa wilaya hiyo Bw. Mtemi Msafiri baada ya kutoridhishwa na utendaji wake. Wametoa ombi hilo jana (Ijumaa, Februari 16, 2018) walipozuia msafara wa Waziri Mkuu alipowasili katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya Kwimba zilizopo Ngudu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Wananchi hao walimkataa mkuu wao wa wilaya Bw. Msafiri kupitia ujumbe wa mabango 17, ambapo Waziri Mkuu amewataka wananchi hao wawe watulivu wakati Serikali inafanyia kazi malalamiko yao. Wananchi hao wanadai kwamba Mkuu huyo wa Wilaya anatabia ya kuamrisha polisi wawakamate kwa kisingizio cha uzururaji na kisha wanawekwa mahabusu, ambapo baada ya muda wanatolewa na kwenda kulima kwenye shamba lake. Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kila mtumishi atambue majukumu yake na ayatekeleze. “Hakuna atakayeonewa, haki zenu zote tunazitekeleza nanyi mnataki...