Kauli ya Zitto Kabwe baada ya kuachiwa
Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23, 2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo.
"Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo" alisema Zitto Kabwe
Aidha Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambapo diwani wa CHADEMA ameauwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali katika mwili wake
"Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia" alisema Zitto Kabwe
Comments
Post a Comment