Zitto Aachiwa kwa Dhamana, Atoa Kauli Mauaji ya Diwani
KIONGOZI Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno ya Sh. 50 milioni na kudhaminiwa na wakili wake, Lazarus Mvula baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi Morogoro tangu jana Alhamisi kwa kufanya mkusanyiko bila kibali. Zitto alikamatwa katika Kata ya Kikeo wilayani Mvomero na alitarajiwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dakawa lakini akahamishiwa Morogoro Mjini.
“Muda huu ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh50milioni. Anatakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018,” inaeleza taarifa ya wakili wake.
Aidha, Zitto amefungukia mauaji ya Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.
Comments
Post a Comment