Posts

Chanzo Cha Maumivu Ya Tumbo Mara Kwa Mara!

Image
Maumivu ya tumbo. MAUMIVU ya tumbo ni tatizo linaloweza kumpata mtu yeyote, mwanamke au mwanaume, mkubwa au mdogo. Maumivu haya husumbua kwani huwa hayaishi, yaani yanatulia kwa muda flani na kurudi tena, aina hii ya maumivu pia inaweza kuwa ya moja kwa moja, yaani hayatulii na wakati mwingine mgonjwa hupata nafuu kwa kujikunja au kushikilia tumbo. Maumivu yanaweza kuwa upande wa juu wa tumbo au upande wa chini na yanatulia kwa vipindi na kurudi yakiwa makali au madogo lakini hayaishi. JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA Kama tulivyoona, humtokea yeyote mwanamke au mwanaume, utokeaji wake hutofautiana kwa jinsi. Kwa mwanaume vyanzo vya maumivu haya vinaweza kuwa hernia au ngiri au matatizo kwenye korodani, lakini kwa wote vyanzo vinaweza kuwa vidonda vya tumbo, matatizo ya mkojo, kidole tumbo, matatizo ya utumbo mkubwa, kukosa au kufunga kupata haja kubwa, gesi kujaa tumboni. Yapo mengine kama kuwa na mawe kwenye mfumo wa mkojo au kifuko cha nyongo, matatizo ya ini na mengi

Professor Jay;Sugu kaniambia niwaambie msiogope endeleeni kupaza sauti

Image
Baada ya Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Professor Jay) kwenda Mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge huyo amesema kuwa Sugu amesema kuwa wasiogope waendelee kupaza sauti. Professor Jay amesema kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo ambapo RCO na RPC wa Mbeya watasimama kutoa ushahidi wao. “SUGU kaniambia niwaambie ‘MSIOGOPE’ bali endeleeni kupaza Sauti!!Kesi yao inaendelea leo saa Tatu asubuhi hii katika mahakama kuu ya Mbeya, ambapo RCO na RPC wa Mbeya watasimama kutoa ushahidi wao LEO,” ameandika Proffesor Jay kwenye ukurasa wake wa Insta. Sugu anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli. Ambayo wanadaiwa kuitoa Disemba 30 kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge.

PUTIN ASEMA: SIJAWAHI KUWA NA ‘SMARTPHONE’

Image
Rais wa Russia, Vladimir Putin (kulia) aliyekiri hana simu ya kisasa (smartphone). Kiongozi huyo aliyewahi kuongoza pia shirika la ujasusi la Urusi ya Kisoviet (KGB) amesema huwatumia wasaidizi wake kumtafutia habari anazotaka. “SINA simu ya smartphone,” ndivyo ambavyo husema Rais wa Russia, Vladimir Putin, kila anapoulizwa iwapo ana simu hizo za kisasa. Licha ya kuambiwa kwamba “kila mtu ana smartphone mfukoni”  huko Siberia, nchini Russia, wakati akiwa ziarani, kiongozi huyo pia aliwahi kusema kwamba hataki kutumia tovuti (website) na aliwahi kukiri kwamba mtandao wa Internet ni kimradi cha shirika la ujasusi la Marekani – CIA – na kwamba nusu ya kazi yake ni kuonyesha ngono. Pamoja na kwamba watu wengi nchini mwake, wakiwemo wanafunzi,  huchakarika ili kupata aina hizo za simu, Putin amefichua kwamba analitawala taifa hilo la watu milioni 144 bila kutumia smartphone. Akiwa amekiri pia kwamba hapendi mambo ya technolojia mpya, amesema kamwe huwa hatumi

Wema apigwa mamilioni ya pesa

Image
Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu. Wiki moja baada ya akaunti ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu kudukuliwa na wajanja wa mjini, mrembo huyo anadaiwa kupigwa mamilioni. Habari zilizolifikia dawati la gazeti hili zilieleza kuwa, tangu mrembo huyo adukuliwe akaunti yake hiyo yenye wafuasi zaidi ya milioni tatu, wajanja hao wamekuwa wakiitumia ndivyo sivyo kwa kuposti matangazo mbalimbali ya kibiashara ambapo wanachukua pesa bila ya Wema kujua. Inaelezwa kuwa, Wema alikuwa akitumia akaunti hiyo kupitia namba ya simu ya mtandao maarufu wa mawasiliano nchini ambapo wadukuzi walifanikiwa kumiliki namba hiyo ambayo hutumia moja kwa moja kuwasiliana na wafanyabiashara mbalimbali wa mtandao kwa mgongo wa Wema na kuvuna pesa. Wajanja hao, kwa siku moja tu hutumia akaunti hiyo kuvuna zaidi ya laki saba ambapo kwa wastani wa tangazo moja huchukua kiasi cha shilingi elfu hamsini hadi laki moja. WATAALAMU WANASEMAJE?

Chanzo Cha Maumivu Ya Tumbo Mara Kwa Mara!

Image
Maumivu ya tumbo. MAUMIVU ya tumbo ni tatizo linaloweza kumpata mtu yeyote, mwanamke au mwanaume, mkubwa au mdogo. Maumivu haya husumbua kwani huwa hayaishi, yaani yanatulia kwa muda flani na kurudi tena, aina hii ya maumivu pia inaweza kuwa ya moja kwa moja, yaani hayatulii na wakati mwingine mgonjwa hupata nafuu kwa kujikunja au kushikilia tumbo. Maumivu yanaweza kuwa upande wa juu wa tumbo au upande wa chini na yanatulia kwa vipindi na kurudi yakiwa makali au madogo lakini hayaishi. JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA Kama tulivyoona, humtokea yeyote mwanamke au mwanaume, utokeaji wake hutofautiana kwa jinsi. Kwa mwanaume vyanzo vya maumivu haya vinaweza kuwa hernia au ngiri au matatizo kwenye korodani, lakini kwa wote vyanzo vinaweza kuwa vidonda vya tumbo, matatizo ya mkojo, kidole tumbo, matatizo ya utumbo mkubwa, kukosa au kufunga kupata haja kubwa, gesi kujaa tumboni. Yapo mengine kama kuwa na mawe kwenye mfumo wa mkojo au kifuko cha nyongo, matatizo ya ini na m

MWANAUME AOA WANAWAKE SITA KWA KULIPWA,SABABU Z A TUKIO HILO HIZI HAPA

Image
mmoja wa Marekani katika Jimbo la Massachusetts ameshtakiwa Mahakamani kwa hati ya makosa ya jinai baada ya kuoa wanawake wengi katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2013.   Mtuhumiwa huyu Peter Hicks, 57, alifanya vitendo hivi huku akilipwa kwa lengo la kuwasaidia wanawake hao kukwepa hatua za kupata nyaraka zote za kuwatambua kama wahamiaji wa nchi hiyo. Inaelezwa kuwa Hicks alioa wanawake 6 katika kipindi hicho chote. Wanawake hao wanaripotiwa kutoka katika nchi za Kusini mwa Afrika na alikuwa tayari ameshaomba haki zote wanazotakiwa kupewa wahamiaji wanne kati yao

MZEE MAJUTO: Niombeeni Jamani, Tezi Dume Si Mchezo!

Image
Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ MKONGWE wa filamu za Kibongo aliye kipenzi cha wengi, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ambaye kwa sasa ni mgonjwa ametoa ya moyoni kuwa bado anaumwa hivyo kuwaomba wasanii wenzake na Watanzania kumuombea. Akizungumza na Star Mix, Mzee Majuto alisema Februari 11, mwaka huu anatarajia kurudi tena katika Hospitali ya Tumaini, Dar alikokuwa amelazwa awali na kuruhusiwa baada ya daktari wake kufiwa ambapo ndiyo ataenda kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tezi dume unaomsumbua.   “Niliruhusiwa Jumamosi iliyopita lakini bado naumwa, tezi dume si mchezo, ninachoweza kuwaambia wasanii wenzangu na Watanzania kwa jumla, waniombee tu,” alisema Mzee Majuto

Hivi Ndivyo Vitu Hatari Vinavyoweza Kuharibu Na Kuvunja Ndoa Ya Wapendanao Katika Familia

Image
WAPENZI wanagombana, ndoa zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye msoto kwa sababu ya ubinafsi. Tunazungumza mengi lakini ukweli ni kwamba endapo kila mmoja atafanikiwa kuushinda ubinafasi, upendo utashamiri kila kona. Ubinafsi una matawi mengi. Mtu anaposaliti, maana yake ametekwa na tamaa binafsi. Anashindwa kutambua kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa hiyo anatakiwa kulinda penzi la mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni dhuluma ya hali ya juu. Ukweli ni kwamba unapoanzisha uhusiano na mtu, maana yake umeamua kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako. Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine, huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za ndani ya mwili wako mwenyewe. Kwa nini ukimfumania mwenzi wako panachimbika? Ni kwa sababu alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako, kwa maana hiyo amekutendea dhuluma. Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana kwa sababu haki yako imetumika ndivyo sivyo. Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umei

Rose Ndauka: Natamani Kuongeza Mtoto Mwingine

Image
Rose Ndauka MUIGIZAJI mwenye mikogo Bongo Muvi, Rose Ndauka amefunguka kuwa anatamani sana kuongeza mtoto mwingine kutokana na raha anayoipata kutoka kwa mtoto wake huyo wa kike aitwaye Naveen lakini bado hajapata wa kuongeza naye. Akizungumza na Star Mix, Rose alisema kuwa, mtoto wake amekuwa akimpa faraja sana kila wakati hivyo kumpa hamu tena ya kuongeza mtoto mwingine ili azidishe furaha aliyonayo sasa. “Kwa kweli nisiwe muongo, natamani sana kuongeza mtoto mwingine maana nishaona ndiyo faraja yangu ila tatizo ni mwanaume wa kuzaa naye sijampata, hata hivyo Mungu ni mwema naamini atapatikana tu,” alisema Rose.

Diamond, Mobeto wamaliza fofauti zoa

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond amesema mazungumzo katika kesi yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto kati yake na mwanamitindo Hamisa Mobeto,  imekwenda vizuri. “Niseme tu mambo yameenda vizuri na kama mnavyojua mambo ya mahakamani ikitokea ninahitajika nitakuja,” amesema. Diamond alifika mahakamani hapo leo Februari 8, 2018  kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prince Abdul iliyofunguliwa na Mobeto. Amesema yeye na Mobeto hawana shida yoyote, ila kuna watu waliokuwa wakizungumza maneno na kumchochea Mobeto. "Tunahitaji kuweka mambo sawa. Tunahitaji kuwa katika mstari kwa sababu vitu vidogo vinaharibu upande wa mama na upande wa baba kwa hiyo tulikuwa tunaweka mambo sawa ili kesho na keshokutwa yasilete sintofahamu baina yetu,” amesema na Diamonda na kuongeza: “Ikitokea kuna mtafaruku baina ya mtoto, kila mtu anakuwa na mawazo yake, kwa hiyo ni lazima kumjenga mtoto na kuhakikisha kuwa mtoto anajengwa na k

ANGALIA WEMA SEPETU ALIVYOFIKA MAHAKAMANI NA WAKILI WAKE,KESI YAKE MAPYA YAIBUKA

Image
Kesi ya mrembo Wema Sepetu ya kukutwa na msokoto wa bangi imesikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Inspekta wa Polisi, Wille ameieleza mahakama kuwa hakuwepo wakati Wema akichukiliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa serikali. Shahidi huyo aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati alipoulizwa maswali na Wakili wa Wema, Alberto Msando. Katika ushahidi wake, Inspekta Wille, alidai hakuwahi kupeleka sampuli za mkojo za washtakiwa wenzake Wema ambao ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Inspekta Wille alidai kuwa February 8, 2017 alifika katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali saa 5 asubuhi na kumkabidhi Mchunguzi Elia Mulima kichupa cha plastiki ambacho ndani kilikuwa na mkojo wa Wema. Wakili Msando alimuuliza Inspekta Wille kama alikuwepo wakati sampuli ya mkojo uliokuwamo ndani ya kichupa cha plastiki unachukuliwa ambapo I alijibu kuwa hakuwapo. Msando alimuhoji

ANGALIA AJIFUNGUA MTOTO KWENYE KORIDO HOSPITALINI

Image
JESICA HOGAN, mama wa watoto sita mkazi wa Riley, Kansas, Marekani, amejifungua mtoto pekee wa kiume katika korido ya hospitali ambayo alikuwa anawahishwa kwenda kujifungua. Mtoto huyo aliyeleta furaha katika familia hiyo ambayo ilikuwa na mabinti mtupu, anaitwa Max, ambaye alizaliwa akiwa salama na mwenye afya njema. Mwanamke huyo aliyejifungulia katika Hospitali ya Via Christi, ya Manhattan, Kansas, alisema alikuwa hana uhakika wa tarehe ya kujifungua, hivyo hakujua ni lini uchungu ungelianza. Alikuwa nyumbani wakati chupa ilipovunjika kunako saa tisa usiku ambapo mumewe, Travis, alimkimbiza hospitali. Mara tu baada ya kuingia katika korido ya hospitali hiyo, Jesica alihisi mtoto alikuwa ameanza kutoka, hivyo akaanza kuvua suruali yake wakati kichwa cha mtoto kilianza kujitokeza. Walianza kusaidia na mumewe hapohapo kwenye korido ambapo alilala chini kabla ya manesi kuja na kumsaidia. “Nilikuwa sifahamu hasa siku halisi ya kujifungua, lakini siku hiyo nilijua im

ANGALIA FARASI AFANYWA MSIMAMIZI HARUSINI,NI VITUKO VYA AJABU

Image
Maharusi wapya walikuwa washitakiwe kufuatia makosa ya kumtembeza farasi bila ruhusa maalum, baada ya Bibi harusi kuamua kumuweka farasi huyo kama mmoja wa wasimamizi wake. Mwanadada Alex Wells, mwenye umri wa miaka 28, alifanya uamizi huo alipokuw akifanya mipango ya harusi yake huko Nottinghamshire, Uingereza ambapo hata mume wake aliafikiana naye. Farasi huyu aliyejulikana kwa jina la Toffee, mwenye umri wa miaka 17 inasemekana pia kwa namna moja au nyingine ndiye aliyeruhusu harusi hiyo kufanyika kwani ni rafiki wa karibu sana wa Bi Harusi. Mume wa Alex, Graham Sales alikiri kukubaliana na hali hiyo kwani hata kwenye maisha ya kawaida ni kama anashindana na farasi huyo ili kupata muda na mkewe. Farsi huyu alikuwa na wakati mzuri wakati wa harusi hiyo kwani aliweza kushiriki katika kupiga picha za pamoja na mambo mengine.    

Breaking News: Tambwe Hizza wa Chadema Afariki Dunia

Image
Kada wa Chadema,  Tambwe Hizza, enzi za uhai wake. KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  Tambwe Hizza, amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake akiwa amelala, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene,  amethibitisha  na kuongeza kwamba mwili wake umepelekwa Hospitali ya Temeke Dar es Salaam asubuhi hii. Kwa mujibu wa Chadema, marehemu Hiza alikuwa kwenye moja ya vikao vya chama hicho hadi jana saa tano usiku wa kuamkia leo. …Akiwa katika moja ya mikutano ya Chadema. Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na  alikuwa pia mmoja wa waratibu wa kampeni za chama  hicho katika jimbo la Kinindoni Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa CUF, baadae alihamia CCM na kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM na 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA.

Uwoya, Aunt Ezekiel Wamchokonoa Shonza

Image
Wolper. DAR ES SALAAM: KITENDO cha wasanii wa filamu, Aunt Ezekiel Grayson Gwantwa ‘mama Cookie’ na Irene Pancras Uwoya kutupia picha mtandaoni zikionesha wakiwa wanaogelea huku maeneo nyeti ya miili yao yakiwa wazi, kimetafsiriwa na wadau mbalimbali ni kama ‘kuishika sharubu’ serikali. Mwanzoni mwa wiki hii, picha za wasanii hao wakiwa ndani ya majakuzi sehemu tofauti na kwa nyakati tofauti zimeleta hisia tofauti kwa jamii huku wengine wakienda mbele kwa kusema kitendo hicho ni kukaidi agizo la Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kupitia naibu waziri wake, Juliana Daniel Shonza aliyepiga marufuku picha za utupu mitandaoni. Aunt Ezekiel. Baada ya kuvuja kwa picha hizo, waandishi wetu waliwatafuta wasanii hao kupitia simu zao za mkononi ili kusikia utetezi wao juu ya jambo hilo. “Picha hiyo niko lokesheni (eneo la kuigizia), sasa sioni kama kuna tatizo kuonesha mtandaoni picha ya namna hiyo,” alisema Irene Uwoya. Kwa upande wa Aunt Ezekiel

EWURA Watangaza Bei Mpya Ya Mafuta Kutumika Februari 7, 2018

Image
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo Februari 7, 2018 huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikipanda. Taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany imesema bei za rejareja zimeongezeka kwa petroli ikiwa ni Sh59 sawa na asilimia 2.70, dizeli Sh46 (sawa na asilimia 2.30), na mafuta ya taa kwa Sh24 (sawa na asilimia 1.17). Amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambazo kwa petroli ni Sh58.57 sawa na asilimia 2.85, dizeli kwa Sh46.48 (sawa na asilimia 2.44) na mafuta ya taa kwa Sh23.75 (sawa na asilimia 1.24). Mchany amesema ongezeko hilo linatokana na bei kuongezeka katika soko la dunia. “Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Januari 3. Bei za mafuta ya taa hazijabadilika kwa sababu hakuna yaliyoingizwa nchini kupitia ba

Mwigulu Avamia Shamba la Bangi, Alichokifanya

Image
WAZIRI wa mambo ya ndani nchini,Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari  sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha. Mwigulu akishirikiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, (RPC)Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapo walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana. Akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa zoezi hilo Mwigulu amesema kwamba serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi. Aidha Waziri Mwigulu amewaambia askari waliokuwa wakishiriki katika zoezi hilo, Mwigulu mbali na kuwapongeza kwa kazi wanayofanya lakini amewaambia kwamba pamoja na kufanikiwa kuteketeza madawa ya kulevya yanayo

Kopa, Msagasumu Kupamba Shindano la Nyonga

Image
WAMAMA wa uswazi na ushuwani leo Alhamisi wanata-rajiwa kuon-eshana matu-mizi ya nyonga kwenye shindano litakalo-fanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. Akizungumza na gazeti hili, mratibu wa tamasha hilo, Maimartha Jesse alisema shindano hilo litasind-ikizwa na burudani kutoka kwa Mfalme wa Uswazi (Msaga-sumu), Malkia wa Mipasho (Khadija Kopa), Jack Simela na wengineo. Sambamba na wasanii hao Maimartha alisema pia kutakuwa na burudani ya ngoma za Kibao Kata na Baikoko kutoka Tanga. Maimartha alisema upande wa ushereheshaji atakuwa yeye mwenyewe akisaidiana na Sakina Liyoka ambao kama kawaida yao watamwaga ubuyu mwanzo mwisho. Katika burudani zote hizo kiingilio kitakuwa shilingi 5000 tu. RICHARD BUKOS

Madiwani watatu Chadema wahamia CCM

Image
 Chadema katika Halmashauri ya Tunduma, wilaya ya Momba mkoani Mbeya kimepata pigo baada ya madiwani wake watatu kuhamia CCM. Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Ayub Mlimba (Mwaka Kati), Simon Mbukwa (Kaloleni) na Amos Nzunda (Mpemba) na walitambulishwa jana mchana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Jumaa Irando. Wakizungumza na Mwananchi madiwani hao waliohamia CCM wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza mwelekeo Tunduma, huku viongozi wake wakitoa amri za kibabe wakitaka wanachama kutozungumza chochote. “Unajua baraza la madiwani Tunduma linaundwa na Chadema, sasa tunapewa maagizo ya nini cha kuzungumza na kusimamia hata kama hayaendani na mahitaji ya wananchi wetu kwa lengo tu la watu wachache ndani ya chama,” alisema Nzunda. Mlimba alisema sababu ya kuhamia CCM ni kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli huku Mbukwa akieleza sababu yake kuondoa Chadema kuwa ni mvutano na mtafaruku

JPM Azindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi

Image
RAIS Dkt. Magufuli leo  Februari6,  2018 amezindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi (Comprehensive Training Center – CTC) kilichopo Mapinga katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani na kusema amesikia kilio cha wananchi wa Mpinga. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho vya kisasa vya kiusalama. Baada ya uzinduzi huo Rais Magufuli aliweza kupata nafasi ya kuongea na wananchi wa eneo hilo na kusema amesikia kilio chao. “Nimesikia kilio chenu nataka niwahakikishie kwamba daraja hili ni muhimu, si muhimu tu kwa ajili ya kituo hiki bali ni muhimu pia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wanaokaa maeneo haya ninauhakika daraja hili kama litatengenezwa litapunguza gharama za ukaaji huku lakini pia litaweza kutumika kama ‘altenative route’ ikitokea siku moja daraja likakatika Mpigi pale juu ambapo lili