ANGALIA WEMA SEPETU ALIVYOFIKA MAHAKAMANI NA WAKILI WAKE,KESI YAKE MAPYA YAIBUKA

Kesi ya mrembo Wema Sepetu ya kukutwa na msokoto wa bangi imesikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Inspekta wa Polisi, Wille ameieleza mahakama kuwa hakuwepo wakati Wema akichukiliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa serikali.
Shahidi huyo aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati alipoulizwa maswali na Wakili wa Wema, Alberto Msando. Katika ushahidi wake, Inspekta Wille, alidai hakuwahi kupeleka sampuli za mkojo za washtakiwa wenzake Wema ambao ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Inspekta Wille alidai kuwa February 8, 2017 alifika katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali saa 5 asubuhi na kumkabidhi Mchunguzi Elia Mulima kichupa cha plastiki ambacho ndani kilikuwa na mkojo wa Wema. Wakili Msando alimuuliza Inspekta Wille kama alikuwepo wakati sampuli ya mkojo uliokuwamo ndani ya kichupa cha plastiki unachukuliwa ambapo I alijibu kuwa hakuwapo.
Msando alimuhoji Inspekta Wille kuwa walikaa kwa muda gani katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Inpekta Wille alidai kuwa hakumbuki. Katika maelezo yake, pia Inspekta Wille alidai yeye hakupekuwa katika chuma anacholala Wema bali alipekuwa katika chumba anachohifadhia nguo na viatu.
Alidai kuwa katika upekuzi walikuta msokoto wa bangi jikoni juu ya kabati, pia walikuta msokoto wa bangi uliotumika ukiwa ndani ya kiberiti dirishani katika chumba wanacholala wafanyakazi wa Wawili wa Wema. Baada ya kueleza hayo, aliiomba mahakama ipokee hati ya ukamataji mali iliyojazwa katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Wema kama kielelezo ambapo mahakama ilipokea.
Kesi imeahirishwa hadi February 26 na 27, 2018 itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Comments

Popular posts from this blog