JPM Azindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi

RAIS Dkt. Magufuli leo  Februari6,  2018 amezindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi (Comprehensive Training Center – CTC) kilichopo Mapinga katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani na kusema amesikia kilio cha wananchi wa Mpinga.

Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho vya kisasa vya kiusalama. Baada ya uzinduzi huo Rais Magufuli aliweza kupata nafasi ya kuongea na wananchi wa eneo hilo na kusema amesikia kilio chao.

“Nimesikia kilio chenu nataka niwahakikishie kwamba daraja hili ni muhimu, si muhimu tu kwa ajili ya kituo hiki bali ni muhimu pia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wanaokaa maeneo haya ninauhakika daraja hili kama litatengenezwa litapunguza gharama za ukaaji huku lakini pia litaweza kutumika kama ‘altenative route’ ikitokea siku moja daraja likakatika Mpigi pale juu ambapo liliwahi kukatika kipindi fulani wakati ndugu zangu Wakwele walikuwa wakichimba mchanga pale mpaka daraja likakatika na likawa limekata usafiri mkubwa” 
Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa;
“Mhe. Kawambwa, Ridhiwani Kikwete na wananchi napenda niwaahidi hili nalibeba mwenyewe ili daraja hili lianze kutengenezwa” alisisitiza Rais Magufuli 

Comments

Popular posts from this blog