ANGALIA FARASI AFANYWA MSIMAMIZI HARUSINI,NI VITUKO VYA AJABU

Maharusi wapya walikuwa washitakiwe kufuatia makosa ya kumtembeza farasi bila ruhusa maalum, baada ya Bibi harusi kuamua kumuweka farasi huyo kama mmoja wa wasimamizi wake.
Mwanadada Alex Wells, mwenye umri wa miaka 28, alifanya uamizi huo alipokuw akifanya mipango ya harusi yake huko Nottinghamshire, Uingereza ambapo hata mume wake aliafikiana naye.
Farasi huyu aliyejulikana kwa jina la Toffee, mwenye umri wa miaka 17 inasemekana pia kwa namna moja au nyingine ndiye aliyeruhusu harusi hiyo kufanyika kwani ni rafiki wa karibu sana wa Bi Harusi.
Mume wa Alex, Graham Sales alikiri kukubaliana na hali hiyo kwani hata kwenye maisha ya kawaida ni kama anashindana na farasi huyo ili kupata muda na mkewe. Farsi huyu alikuwa na wakati mzuri wakati wa harusi hiyo kwani aliweza kushiriki katika kupiga picha za pamoja na mambo mengine.   

Comments

Popular posts from this blog