Rose Ndauka: Natamani Kuongeza Mtoto Mwingine


Rose Ndauka
MUIGIZAJI mwenye mikogo Bongo Muvi, Rose Ndauka amefunguka kuwa anatamani sana kuongeza mtoto mwingine kutokana na raha anayoipata kutoka kwa mtoto wake huyo wa kike aitwaye Naveen lakini bado hajapata wa kuongeza naye.

Akizungumza na Star Mix, Rose alisema kuwa, mtoto wake amekuwa akimpa faraja sana kila wakati hivyo kumpa hamu tena ya kuongeza mtoto mwingine ili azidishe furaha aliyonayo sasa. “Kwa kweli nisiwe muongo, natamani sana kuongeza mtoto mwingine maana nishaona ndiyo faraja yangu ila tatizo ni mwanaume wa kuzaa naye sijampata, hata hivyo Mungu ni mwema naamini atapatikana tu,” alisema Rose.

Comments

Popular posts from this blog