Posts

Majaliwa amuagiza CAG kuchunguza mfuko wa CDTF

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa. Majaliwa agizo hilo leo wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma. Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB). Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo zitafanywa na Bodi ya Kahawa. Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.

Mbunge Haonga afichua kuwa wabunge wanajiuza

Image
Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe kwa tiketi ya (CHADEMA), Pascal Haonga amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wabunge wamekuwa wakijiuza na kununuliwa kwa bei ndogo na kudai yeye hawezi kuwa sehemu ya watu hao ambao wananunuliwa. Haonga amesema hayo alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake la Mbozi na kusema wabunge na wanasiasa ambao wana hama vyama kwa kununuliwa na kujidai wanaunga mkono utendaji wa Rais wana upungufu wa akili. "Mimi siwezi kufanya kama wabunge wengine huko ambao wamekua wakijiuza kwa bei ndogo, mmesikia madiwani wananunuliwa, wabunge wananunuliwa. Hivi inangia akilini kweli wananchi walikuchagua na wengine walichoma nyumba za wengine, wengine waliamua kuchoma na magari, wengine waliamua kuchoma na mahakama, baiskeli na Pikipiki halafu unakuja kusema eti namuunga mtukufu kwa jitihada na kazi anazofanya. Hivi wewe Mbunge utakuwa na akili au matope" alihoji Haonga Mbali na hilo Mbunge huyo amewaeleza wananch

Maneno ya Uhuru Kenyatta na Odinga baada ya Olunga kuwa Mkenya wa kwanza kufunga Hat-trick

Image
Michael Olunga amekuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi kuu ya Uhispania ~La Liga. Olunga amefunga magoli matatu (Hat-trick) dhidi ya Las Palmas na kuweka rekodi ya kuwa Mkenya wa Kwanza kufunga hat-trick kwenye Laliga. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kuona taarifa hiyo hakukaa kimya kupitkia ukurasa wake wa Facebook akampongeza Michael Olunga kwa kusema “Ongera Michael Olunga kwa kuweka historia kuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi ya Hispania La Liga na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwa klabu ya Girona katika ligi ya Spain” Nae kiongozi wa Muungano wa Upinzania nchini Kenya Raila Odinga amepost katika ukurasa wake wa Twitter kumpongeza Olunga.  

Kumbe bila kuitwa na Waziri tusingejua Gigy ana mimba

Image
Msanii Gigy Money ambaye hivi karibuni ameonekana akiwa mjamzito na kuwashangaza wengi, amesema hakukusudia kuwajulisha watu bali ilikuwa kwa bahati mbaya wamejua Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv pia Gigy Money amewataka watu kumshukuru Naibu Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo Juliana Shonza kwa kumuita, kwani bila wito huo watu wasingemuona mtaani na kumuona akiwa na ujauzito wake. “Kwanza Mumshukuru yule waziri la sivyo msingeuona, huwa sipendi kabisa kuongelea masuala ya ujauzito wangu ila siku ile ilitokea bahati mbaya watu wakauona, alafu hao wanaosema nimeweka mimba feki ili serikali inionee huruma mi nina undugu na serikali? Kama mtoto anaokotwa basi subirini nami wangu nitamuokota”, amesema gigy Money. Kauli hiyo ya Gigy Money imekuja siku chache baada ya watu kumuona na ujauzito, huku wengine wakidai ameweka mimba feki ili serikali imuonee huruma.

Rais Magufuli ammwagia sifa Kagame

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame atalisaidia bara la Afrika kusonga mbele kimaendeleo kwa kuwa kiongozi huyo anajua matatizo na shida za nchi nyingi za Afrika. Magufuli amesema hayo leo Januari 14, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo yake na Rais Kagame ambayo yamefanyika leo Ikulu na kusema kuwa Kagame ni mwanamapinduzi wa kweli wa Afrika hivyo atakavyokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika atalisaidia bara hilo kusonga mbele zaidi. "Kagame atakapokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) sisi Tanzania tumeipokea hii kwa raha sana kwa sababu tunamfahamu Rais Kagame lakini pia ni jirani yetu mwema sasa Mwenyekiti atakuwa anatoka ndani ya East Africa Community, nimemuakikishia kuwa sisi Tanzania tutampa ushirikiano wa hali ya juu sana katika nafasi hii atakayokwenda kuichukua na nimemthibitishia kutokana na ushawishi wake Afrik

Pombe Za Johari Ilikuwa Stresi

Image
J OHARI amefunguka kuwa pombe alizokuwa akinywa zilikuwa zikichangiwa na msongo wa mawazo. Johari ameliambia Spoti Xtra kuwa kutokana na ugumu wa kazi za filamu kwa hivi sasa lazima mtu uchanganyikiwe nini kifanyike ili filamu zisife. “Wakati mwingine nilikuwa nakunywa pombe sana kwa ajili ya msongo wa mawazo lakini niliona sio suluhisho kunywa pombe,” alisema Johari.

BAADA YA UBINGWA WA MAPINDUZI CUP, AZAM FC IMECHUKUA MAAMUZI HAYA KUHUSU SURE BOY…

Image
Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Azam Fc imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, hiyo ni baada ya kuifunga URA ya Uganda kwa penati 4-3. Awali katika dakika 90 za mchezo huo, timu hizozilitoka suluhu ya 0-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, jana usiku kisiwani Unguja. Baada ya kukabidhiwa ubingwa huo, taarifa kutoka Azam FC zinaeleza kuwa ubingwa huo wameutoa zawadi kwa kiungo wa timu hiyo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, na hii ni baada ya kufiwa na Mama yake mzazi wiki iliyopita wakati akiwa na timu hiyo kwenye harakati za kuwania taji hilo. Hadi Azam FC inatwaa ubingwa, imeweza kucheza jumla ya mechi sita, ikishinda mara tano na kupoteza mmoja huku ikiruhusu nyavu zake kuguswa mara moja tu, na hii ni walipofungwa bao 1-0 dhidi ya URA kabla ya kulipa kisasi kwenye mchezo huo wa fainali. Kikosi hicho kilitarajiwa kuondoka visiwani Zanzibar, asubuhi ya leo Jumapili kurejea jijini Dar es Salaam tayari kabisa kuanza maandalizi ya kuwakabili Majimaji

KAULI YA ALBERTO MSANDO KUHUSU SAKATA LA LEMUTUZ LILILOTIKISA MTANDAONI

Image
From @albertomsando -Kaka na rafiki yangu @lemutuz_superbrandtz; Nimetamani sana nikae kimya upambane na ‘msala’ wako mwenyewe. Lakini nimeshindwa. Nimeshindwa kwa sababu naelewa na najua inavyokuwa pale unapopitia unachopitia. I have been there. Niseme kwamba kwa comments zote unaweza sasa kuelewa kiasi cha chuki dhidi yako. Kiasi cha furaha kwa maadui zako. Lakini ndani yake usiache kuona kiasi kidogo cha upendo na huzuni kutoka kwa marafiki zako. Kosa lako ni kuruhusu kile ambacho wengi wanafanya kufika hadharani kwa kuwa karibu na kumpa nafasi aliyefikisha. Hilo ndio kosa lako la kwanza. “Kosa” la pili ni unavyoishi. Umeamua kuishi maisha yako vile ambavyo wewe mwenyewe umechagua. Kuna wengi wanakereka bila hata sababu. Ni maisha yako! Kosa sio ‘kibamia’ au kujifuta ulipotoka kuoga. Wengi sana wana ‘vibamia’ na wanaoga na kujifuta. Wengi wamekutana navyo na wanaishi navyo. Wala hakuna kosa kuwa na kibamia. Utu na heshima yako ni zaidi ya kila kitu. Ni huzuni

BREAKING NEWS: Rais Magufuli afanya mazungumzo na Lowassa Ikulu

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi kwa Watanzania. “Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo. “Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote ina

Chid Benz Adakwa na ‘Unga’

Image
NGULI WA wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro ‘Chid Benz anashikiliwa tena  na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na hii inakuwa mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili. Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP, Giless Muroto amesema kwamba ni kweli msanii huyo alikamatwa na taarifa kamili zitatolewa hapo kesho. Kamanda Muroto amesema; “ Ni kweli Chidi Benz mnamo Desemba 30, 2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zidhaniwayo kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani “ Aidha ameongza kuwa watuhumiwa wote bado wako mahabusu.

Hizi ndizo sababu nyimbo za Lady Jaydee kutochezwa Clouds

Image
Lady Jaydee ameeleza kuhusu nyimbo zake kushindwa kuchezwa Clouds Media wakati ilionekana tayari wameshamaliza bifu lao. Akiongea na Dizzim Online msanii huyo amesema, hajawahi kukataza nyimbo zake kuchezwa na kituo hicho hata hivyo walisharuhusiwa na Seven lakini hakuna kilichofanyika. “Ilisemekana kuwa mimi ndio nilikataza nyimbo zangu kupigwa, jambo ambalo sio kweli. Mimi sikukataza nyimbo zangu kupigwa na hakuna sehemu yoyote niliyoandika nyimbo zangu zisipigwe, wao ndio waliamua kwa sababu kuongea kwangu kule kwamba nyimbo zisipigwe. Baada ya hapo walisema akitoa ruhusa nyimbo zake zipigwe zitapigwa. Seven aliongea na akatoa Go ahead je walipiga? Kwa hiyo hapo sio tatizo langu mimi, hapo inadhihirika wazi kabisa kuwa tatizo liko wapi na mtu anaweza kuongea kitu sio kwa kumaanisha,” amesema Jide. Mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2016 Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alipokuwa akiongea na kipindi cha XXL alisema

Kumbe aliyejiunganishia bomba la mafuta ni mstaafu wa Tazama

Image
Aliyejiunganishia bomba la mafuta nyumbani kwake Samwel Kilanglani(63) amejulikana kuwa ni mfanyakazi mstaafu wa bomba la kusafirisha mafuta Tanzania na Zambi (Tazama). Kilanglani anatuhumiwa kutoboa bomba la mafuta ya dizeli la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) na kujiunganishia kwenye mantaki mawili yakiwa ndani ya nyumba yake iliyopo Tungi Kigamboni. Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika amesema mtuhumiwa huyo alijiunganishia na bomba la TPA kwa njia ya kuchomelea na kuunganisha moja kwa moja kwenye mantaki yake mawili yaliyochimbiwa chini ndani ya nyumba yake. Kitalika amesema mtuhumiwa alijiunganishia katikati na bomba kuu hivyo mafuta yanapopelekwa sehemu husika mengine yanaingia kwake hivyo hayafiki kama yalivyokusudiwa. "Mafuta yanaweza yakapelekwa lita 4,000 sehemu husika lakini hayafiki yote mengine yanaenda kwa mtuhumiwa huyu matokeo yake wanajiuliza haya mengine yameenda wapi,&

Muslim Hassanali Ajiunga CCM Akitokea Chadema

Image
Muslim Hassanali, aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ilala 2015. ALIYEKUWA mgombea ubunge Jimbo la Ilala kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa 2015, Muslim Hassanali, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi  (CCM)  na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula (katikati)akiwa na viongozi wengine. Kujiunga kwa Hassanali ni mwendelezo wa mfululizo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani kuondoka na kwenda CCM. Muslim Hassanali (kushoto) akirudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi mkuu wa  2015. Viongozi kadhaa wakiwemo wabunge na wapinzani wamejiunga na CCM wakitokea upinzani kwa sababu mbalimbali  ikiwemo ya kuunga mkono serikali ya Rais John Magufuli.

Siri 3 Dereva Wa Lissu Kutimkia…

Image
Simon Bakari akiongea na Freeman Aikaeli Mbowe. SIRI tatu za dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Simon Bakari (pichani) kwenda Ubelgiji na bosi wake zimevuja. Mbunge mmoja ndani ya chama hicho aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa chama wala familia, alisema kamati maalum inayoratibu matibabu ya Lissu iliyokutana jijini Nairobi, Kenya iliona ni vema Simon aongozane na bosi wake pamoja na mkewe mbunge huyo, Alicia kwa kuwa ndiye aliyefanya kazi kubwa ya kumuuguza akiwa Nairobi akisaidiana na Mkuu wa Idara ya Uenezi, Hemedi Ali. Tundu Lissu (Chadema). “Pamoja na ukweli kwamba dereva Simon alikuwa ana matatizo ya kisaikolojia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana akiwa na Lissu mkoani Dodoma Septemba 7, mwaka jana, alijitahidi kutoa huduma zisizo za kitabibu pamoja na Hemedi (Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi, Chadema) Nairobi ndiyo maana kamati maalum ya kuratibu tiba ya mbunge huyo ikaona ni vema

Mfungwa afufuka akiwa mochwari

Image
Mfungwa mmoja amezinduka na kujikuta yupo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti baada ya madaktari watatu kuthibitisha kuwa alikuwa amefariki, vyombo vya habari Uhispania vimetoa taarifa hiyo. Gonzalo Montoya Jiménez alikuwa ni mfungwa katika gereza Asturias na alizinduka saa chache  kabla ya kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kugundua chanzo cha kifo chake. Gonzalo yupoa chini ya uangalizi wa madaktari katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Oviedo. Mmoja wa ndugu zake ameliambia gazeti la La Voz de Asturias kwamba Gonzalo  “alikuwa amewekewa alama ya kufanyiwa upasuaji, tayari kupasuliwa”. Wataalamu wamesema hali hiyo inaitwa ‘catalepsy’ ni hali ambayo ishara muhimu za uhai hufifia kwenye mwili wa binadamu kiasi cha kutoweza kutambulika kama yupo hai.

Kingunge Ataka Kujua Hali ya Tundu Lissu

Image
Aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa (wa pili kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe,   wakimjulia hali  Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili. MWANASIASA mkongwe , Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili kufuatia kung’atwa na mbwa amemkumbuka na kutaka kujua haliya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye amesafirishwa kutoka hospitalini Nairobi, Kenya,  kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi. Kigunge ameulizia hali ya Tundu Lissu baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa aliyekuwa amefuatana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,  Edward Lowassa,  walipomtembelea leo Januari 8, 2018 katika hospitali ya Muhimbili. “Vipi hali ya  Tundu Lissu? Nimeona mimi jinsi wanavyonifanyia hapa (madaktari),  nimewauliza mimi tu niliyeng’atwa na mbwa mnanifanyia hivi, je Lissu mmemfany

Lowassa, Mbowe wamtembelea Kingunge Hospitali

Image
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa kumjulia hali Mzee Kingunge Ngumbare Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili anapopatiwa matibabu. Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake . Hivi karibuni Rais John Magufuli alifika hospitalini hapo kumjulia hali Kingunge ambaye ni miongoni mwa wazee wakongwe kwenye siasa za Tanzania ambaye amewahi pia kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini tangu awamu ya kwanza hadi ya nne.

RAIS MAGUFULI AANIKA MADUDU ZAIDI WIZARA YA MADINI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanika madudu mengine ya Wizara ya Madini akisema kuwa baadhi ya wateule wake katika wizara hiyo wamekuwa wazembe katika kutekeleza maagizo na kutimiza majukumu yao kama watendaji wa serikali. Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais ametolea mfano wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa bungeni mwezi Julai mwaka jana, ambapo amesema mpaka sasa wizara hiyo haijapitisha kanuni (regulations) ili sheria hiyo iweze kufanya kazi jambo ambalo amesema ni uzembe usiovumilika huku akimwagiza Waziri wa Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kukamilisha kanuni hizo na kuzisaini kufikia Ijumaa ya wiki hii. “Nakushukuru Mhe spika kwa kutoa ushauri kwa serikali na sisi tumekuwa tukiufuata sana. Wizara ya madini ina changamoto sana na hata sasa ina changamoto na haifanyi kazi vizuri. Spika utakumbuka mwezi wa saba mlifany

RAIS ABAINI MADUDU TENA BANDARINI, ATEUA KAMISHNA WA MADINI

Image
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kuwa Kamishna wa Madini. Rais ametangaza uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa hotuba fupi mara baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini. Nimesikia tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna mpya wa madini, jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo atakuwa ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa madini. Mambo ya hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume kasirisiri hivi, kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi. Yanayogundulika huko ni ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo makontena bandarini na pale Ubungo. Mimi sio mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata wakubembeleza, ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za sheria ya madini) ziwe zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni mkazifanyie kazi, tafuta watu wa kukusaid

BREAKING NEWS: NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARALA LA NNE

Image
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifaulu vizuri katika mitihani hiyo. Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu, Januari 8, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo. Amesema wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha. Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu. Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwaweze