Lowassa, Mbowe wamtembelea Kingunge Hospitali

Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa kumjulia hali Mzee Kingunge Ngumbare Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili anapopatiwa matibabu.

Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake .

Hivi karibuni Rais John Magufuli alifika hospitalini hapo kumjulia hali Kingunge ambaye ni miongoni mwa wazee wakongwe kwenye siasa za Tanzania ambaye amewahi pia kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini tangu awamu ya kwanza hadi ya nne.

Comments

Popular posts from this blog